Kikao cha kupima  uwezo wa kijeshi na silaha za nyuklia za Korea Kaskazini, kilifanyika Jumapili ya jana kwa kuhudhuriwa na Kim Jong-un, Kiongozi wa nchi hiyo mjini Pyongyang.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimeripoti kwamba katika kikao hicho kulijadiliwa mwenendo wa kuimarishwa uwezo wa jeshi la nchi hiyo dhidi ya vitisho vya kijeshi vinavyoikabili nchi hiyo. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuimarishwa siasa za kujilinda kijeshi katika uga wa nyuklia wa Korea Kaskazini na kuandaliwa stratijia ya kujiweka tayari kikamilifu jeshi la nchi hiyo, ni maudhui nyingine zilizojadiliwa katika kikao hicho. 

Aidha kikao hicho kiliamua kuzidisha uwezo wa vikosi vya mizinga nchini Korea Kaskazini.