Afisa wa polisi anaetuhumiwa kwa mauwaji ya Mmarekani mweusi, George Floyd atiwa mbaroni na kushtakiwa kwa kosa la mauwaji kufuatia kifo cha bwana huyo ambae hakuwa na silaha.

 
Hayo yanatokea katika kipindi ambacho mamlaka zikitangaza marufuku za kutotoka nje baada ya vurugu za maandamano ya siku tatu ambazo zimesababisha baadhi ya maeneo kuchomwa moto. Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu ambae alichukuliwa video, ikionesha kambana kwa kutumia goti shingoni, marehemu George Floyd kwa karibu dakika tisa, anashitakiwa kwa kusababisha kifo pasipo kukusudia na mauwaji kwa kizembe.


Ndugu wa marehemu aliyekuwa na umri wa miaka 46, ambao hapo jana walizungumza na Rais Donald Trump, wameonesha kuridhishwa na hatua ya kukamatwa kwa afisa huyo kama uelekeo wa upatikanaji wa haki, lakini pia walisema wana matumaini ya kufunguliwa zaidi kwa mashitaka makali na hatua dhidi ya maafisa wengine ambao wamehusika na kumweka kizuizini Floyd na hatimae kifo chake.


Habari za kukamatwa kwa kushitakiwa kwa askari hiyo kunafanyi amuda mfupi baada ya gavana wa Jimbo Minnesota Tim Walz akiwataka wananchi kuachana na maandamano kwa ahadi ya kupatikana kwa haki katika kesi hiyo mpya. Walzi pia alisema hakutakuwa na mtiriko mzuri wa upatikanaji haki kuendelea kuwepo kwa vurugu. "Moto bado unawaka katika mitaa yetu. Hali ya uchungu inajidhihirisha katika uso wa ulimwengu na dunia inalitazama jambao hili."

Hata hivyo Walz anasema walinzi wa jimbo watafanya kazi ya kurejesha hali ya utulivu baada ya siku tatu ya vurugu za uchomaji moto na uharibifu. Awali Ijumaa, Rais Donald Trump aliwatishia waandamanaji aliowaita vibaka kwa katika viunga vya Minneapolis kwa mtutu wa bunduki, akisema wakati vibaka wakianza na risasi zitaanza.