Kenya imefunga kwa muda wa siku 30 mipaka yake ya kimataifa kuenda Tanzania na Somalia kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi Mei 16. Katika hotuba yake kwa taifa Rais Uhuru Kenyatta amesema hatua hiyo inajumuisha udhibiti usafiri wa watu kutoka mataifa hayo kuingia nchini Kenya.
Hatahivyo usafirishaji wa mizigo utaindelea kati ya Kenya na mataifa hayo mawili.
Marufuku hiyo ya kuzuia watu kutoka Tanzania na kuingia nchini Kenya inaanza usiku wa leo saa 6 na kuruhusu mizigo tu kupita.
Na kwa upande wa Somalia masharti ni hayo hayo, mizigo peke yake ndio itaruhusiwa.
Aidha madereva watakaoingia nchini Kenya kuleta mizigo watatakiwa kupima corona kwanza.
Kenya imeongeza tena muda wa marufuku ya kutoka nje kwa muda wa siku 21.
Kufikia sasa idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 830 baada wagonjwa wapya 49 kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Waliofariki kutokana na corona ni watu 50 baada ya wengine watano kufa.
Rais Kenyata pia ametangaza kuwa wagonjwa 17 wametolewa hospitalini walipokuwa wakipata matibabu.
Rais Kenyatta pia ameongeza muda wa watu kutoka nje wa kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi hadi Juni 6,2020.
”Najua Wengi wanataka maisha yarudi kama vile ilikuwa lakini wenzagu sitaki niwadanganye. Jukumu la kwanza la serikali ni kulinda maisha ya Wakenya”, alisema.
Marufuku ya usafiri kuingia na kutoka miji mitano ikiwemo Nairobi, pia imeongezwa kwa siku 21.
Madereva 25 kutoka Tanzania wamezuiwa kuingia Kenya
Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Kenya madereva hao walipimwa na kupatiwa matokeo yao katika kipindi cha saa 24 kwenye mpaka wa Namanga.
Serikali ya Kenya imesema kwamba hatua ya kuzuia madareva hao kuingia nchini humo inalenga kuwalinda Wakenya dhidi ya maambukizi kutoka kwa raia wa kigeni.
Katika mkutano wake na wanahabari katibu tawala wa waziri wa Afya Rashid Aman aliongezea kwamba maabara mbili za kuhama hama zitazinduliwa katika mpaka wa Namanga ili kuimarisha upimaji wa wagonjwa wapya.
Chanzo BBC.
The post Kenya yafunga mipaka yake upande wa Tanzania na Somalia kwa siku 30 appeared first on Bongo5.com.