Wizara ya Afya Kenya imesema wagonjwa wengine wapya wa corona 23 wameongezeka na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 672 nchini humo. “tumepima sampuli 1,056 ndani ya saa 24 na Watu 23 wana corona, kati yao Wanaume ni 13 na Wanawake 10, mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka mmoja na miezi tisa na mkubwa ana miaka 80”

Wizara hiyo imesema licha ya maambukizi ya corona kufikia 672 nchini humo, wagonjwa wawili wa corona wote kutoka Mombasa wamefariki na kufanya idadi ya vifo vya corona kufikia 32, wagonjwa wengine 32 wemepona na kufanya idadi ya waliopona corona hadi sasa Kenya kufikia 239.

The post Kenya visa vipya vya Corona 23 jumla 672, wamepona 239 na jumla ya vifo ni 32 appeared first on Bongo5.com.