Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini TFF Wilfredy Kidau amehojiwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa .

Katibu mkuu huyo aliingia katika chumba cha mahojiano saa tatu na dakika 42 na kutoka saa tano na dakika 14.

 Baada ya kutoka ndani  Kidao hakutaka kuongea chochote na waandishi wa habari.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa TAKUKURU Brig. John Mbungo aliweka wazi kuwa wanaendelea kuwahoji watu mbalimbali kuhusu matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali.