HOTUBA YA MHESHIMIWA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. PHILIP I MPANGO (MB), KWENYE HAFLA YA KUPOKEA SEHEMU YA MALIPO YA FIDIA, DODOMA, 26 MEI 2020


1.         Utangulizi

Tukio hili la leo ni mwanzo wa safari muhimu katika utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa msingi kati ya serikali ya Tanzania na ya Barrick yaliyofikiwa tarehe 19 Disemba 2019 na kusainiwa rasmi tarehe 24 Januari 2020 jijini Dar es Salaam.

Masuala muhimu yaliyokubalika na kila upande ni:

(i)      Kuunda Shirika la Madini la madini la Twiga lenye umiliki wa pamoja  litakayofanya kazi nchini katika kusimamia uendeshaji wa migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara pamoja na migodi mingine nchin ambapo serikali ya Tanzania itashiriki katika utoaji wa maamuzi kuhusu uendeshaji wa migodi, mipango, manunuzi pamoja na masoko ya madini. Shirika la madini la Twiga lilizinduliwa rasmi 20, octoba 2019.
(ii)     Nia ya Kampuni ya Barrick ni kufanya kazi na Serikali ya Tanzania katika maeneo ya uchambuzi yakinifu juu ya jinsi nchi inavyonufaika na maendeleo ya uchakataji wa madini (Smelter facility)
(iii)    Faida za kiuchumi zitokanazo na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi pamoja na North Mara zigawanywe kwa msingi wa usawa kati ya washirika yaan 50/50 ambapo hisa za Serikali zinazotokana na faida za kiuchumi zitatolewa katika mfumo wa mrahaba, kodi pamoja na kupata asilimia 16 ya faida kutokana na makampuni hayo kufanya kazi nchini.
(iv)   Barrick kulipa dola milioni 300 za kimarekani kwa Serikali ya Tanzania kama malipo ya Patano kuhusu fidia  ya kodi kutokana na makubaliano yaliyofikiwa.
(v)     Serikali ya Tanzania kuruhusu usafirishaji wa Makinikia nje ya nchi.

2.         Chimbuko:

Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana

Utakumbuka kuwa Tanzania ilipitisha sheria muhimu tatu mwezi Julai 2017 ambazo zilitoa muelekeo wa sekta ya madini, sheria hizo ni:

(1)   Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya Mwaka 2017 (Sheria ya Madini Sura ya 123);
(2)   Sheria ya Umiliki wa Maliasili na Rasilimali ya Mwaka 2017; na
(3)   Sheria ya Mapitio ya Masharti Hati katika Mikataba ya Maliasili na Rasilimali ya Mwaka 2017.

Kufuatia mabadiliko katika sekta ya madini,  majadiliano kati ya GNT na kampuni ya Barrik yalianza jijini Dar Es Salaam tarehe  31 Julai 2017. Kufuatia  hoja za msingi za Serikali,  majadiliano yalifanyika kupitia  jitihada za utekelezaji wa azimio la Profesa John Thornton’s wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa washikadau kwamba:
Kanuni za msingi za BGC’s  zinatokana na uelewa na jitihada za pamoja katika karne ya 21 kama jambo la msingi katika kujenga ushirikiano wa kina na kuaminiana na Serikali wenyeji, jamii , Mashirika yasiyo ya kiserikali, wazawa pamoja na wadau wengine.  Kutokana na kuhusishwa kwa watu hao muhimu, tunaruhusiwa kuchukua madini yao nje ya wigo wa utawala wao na hivyo kuwezesha utajiri kwa wote’
Baada ya miaka miwili ya majadiliano, tarehe 24 Januari 2020, mikataba na nyaraka zifuatazo ziliwekwa saini.
     Rasimu ya Mkataba wa Makubaliano ya Msingi (Framework Agreement);
(i)                 Mkataba ya Uchimbaji Madini kwa mgodi wa Bulyanhulu uliorekebishwa (Mining Development Agreement);
(ii)         Mkataba ya Uchimbaji Madini kwa mgodi wa North Mara uliorekebishwa;
(iii)        Mkataba ya Uchimbaji Madini kwa mgodi wa Buzwagi uliorekebishwa;
(iv)       Mkataba wa Wanahisa katika Kampuni ya Ubia baina ya Serikali na Barrick (Shareholders Agreement);
(v)         Mkataba wa Wanahisa katika Kampuni ya North Mara, ikiwemo Serikali;
(vi)       Mkataba wa Wanahisa katika Kampuni ya Bulyanhulu, ikiwemo Serikali;
(vii)      Mkataba wa Wanahisa katika Kampuni ya Buzwagi, ikiwemo Serikali;
(viii)     Mkataba wa Menejimenti na Huduma za Uendeshaji wa makampuni tanzu;
(ix)        Katiba ya Kampuni ya Ubia baina ya Serikali na Barrick (Memorandum and Articles of Association);
(x)         Katiba ya Kampuni Tanzu ya Bulyanhulu iliyorekebishwa;
(xi)        Katiba ya Kampuni tanzu ya North Mara iliyorekebishwa; na
(xii)        Katiba ya Kampuni tanzu ya Buzwagi iliyorekebishwa.

3: Kuhusu Kanuni ya 50/50
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana.
Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick zimekubaliana kwamba pande mbili zitashirikiana katika msingi wa mambo yote  yanayohusisha faida za kiuchumi zinazotokana na madini ya Tanzania katika msingi wa 50/50 kwa kuzingatia mipango ya uwepo wa madini inayoendana na kanuni ya usawa wa kiuchumi kama ilivyoelezwa na sheria. Itakumbukwa kwamba malipo ya dola za kimarekani milioni 300 ni nje ya kanuni ya 50/50.

4.0. Kuhusu Malipo ya mwanzo ya Dola za Kimarekani milioni 100

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana

Hundi ya Dola za Kimarekani milioni 100 inayotolewa leo ambayo ni sawa na kiasi cha Shilingi bilioni 250 ni sehemu ya malipo ya awali ya kiasi cha Dola za Marekani milioni 300 sawa na kiasi cha shilingi bilioni 750. Pande husika zimekubaliana mpango wa malipo wa bakaa ya kiasi cha Dola za Marekani milioni 200.

Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Kampuni ya Barrick kwa kuonesha dhamira ya dhati ya ushirikiano mzuri kwenye muelekeo mpya wa sekta ya madini Tanzania ambao umekubalika na pande zote kwa manufaa ya pande zote husika.

5.           Ahadi za Kiuchumi na Kijamii zilizotolewa

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,

          Mbali ya makubaliano hayo, Kampuni ya Barrick imekubali kufanya yafuatayo:

(i)        Kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 5 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Mtambo wa kuchaka madini nchini (Smelter);
(ii)       Kuanzisha ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoa hadi dola za marekani milioni 10 kwa kipindi cha miaka kumi kwa ajili ya utoaji wa mafunzo yanayohusu sekta ya madini;
(iii)      Kutoa hadi dola za marekani 6 kwa kila ounce ya madini itakayouzwa (ikijumuisha mchango kwenye Mfuko wa Maendeleo ulioanzishwa na Kampuni ya Barrick Tanzania) ili kusaidia jamii zinazozunguka maeneo ya migodi;
(iv)     Kutoa kiasi cha dola za marekani milioni 40 kwa ajili ya kuboresha kipande cha barabara kati ya Bulyanhulu na Mwanza na kujenga nyumba na miundombinu yake;

6.         HITIMISHO:

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,

Tunatumaini kwamba, pande zote mbili zinazohusika katika makubaliano zitaheshimu makubaliano na kuhakikisha yanatekekelezwa. Nawahakikishia kwamba, kwa upande wa Serikali ya Tanzania imedhamiria kwa dhati kutekeleza makubaliano hayo. Na kama ilivyoshuhudiwa hivi karibuni Serikali imeruhusu makontena na makinikia ya madini 277.

Tukio la leo ni hatua muhimu katika Sekta ya madini nchini ikizingatiwa kuwa Kampuni ya Barrick ni mdaiu muhimu katika Sekta hii. Nawaomba Kampuni nyingine za madini na wawekezaji wengine katika Sekta hii kufuasta mfano mzuri uliooneshwa na Kampuni ya Barrick katika kuhakisha kunakuwa na hali ya usawa (win- win Situtuation) katika uendeshaji wa shughuli za madini.

Napenda kuhitimisha kwa kutangaza kwamba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania imedhamiria kwa dhati kuwa ushirikiano wenye usawa katika Sekta ya madini utasaidia kuleta fedha ambazo zitasaidia katika kuboresha maisha ya Watanzania.


Ahsanteni kwa Kunisikiliza
______________