Msanii wa muziki Kala Jeremiah ambaye ni zao la BSS mwaka 2006, amefunguka mengi yanayozungumzwa kuhusu zawadi wanazopewa washindi wa BSS huku akijinadi kwamba yeye licha ya kushika nafasi ya nne ya mashindano hayo ya mwaka 2006 na kupewa zawadi ya komputa, meza ya komputa pamoja na deki lakini mashindano hayo yaliweza kubadili maisha yake.
“Mimi kama mshindi wa nne mwaka 2006 zawadi zangu zilikuwa ni komputa, meza ya komputa pamoja na deki na vitu vyangu vyote nilivipata kwa wakati na kusema kweli mpaka sasa deki ninayo” alisema Kala.
The post Kala Jeremiah aibuka na ishu ya BSS “Nilipewa zawadi ya kompyuta na deki tu lakini…” appeared first on Bongo5.com.