Msanii wa muziki na Rais wa label ya African Boy, @juma_jux amesema yeye ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania anayelipa kodi kubwa kupitia biashara yake ya nguo.

Akinguzungumza na @iambenpol kupitia Insta Live, Jux alikuwa anazungumzia mafanikio ya bidhaa zake za nguo za African Boy.

“Mimi ni mmoja kati ya wafanyabishara na wasanii ambao wanalipa kodi kubwa, mimi kontena yangu moja nalipa tsh milioni 26 mpaka 27 na kwa mwaka naingiza kontena mbili mpaka tatu,” alisema Jux.

Jux amesema kwa sasa ana duka la jumla Kariakoo Tanzania pamoja na Uganda huku akiwa na malengo ya kutanua biashara yake Afrika na duniani.

Muimbaji huyo amesema kwa sasa biashara hiyo anaimilili kwa asilimia mia moja huku akisema biashara ikitanuka na kuanza kuzaa matunda zaidi ataanza kuuza hisa.

The post Jux adai kupitia biashara ya African Boy analipa kodi ya tsh millioni 81 kwa mwaka appeared first on Bongo5.com.