Mgombea urais nchini Marekani katika tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden, amekanusha vikali madai ya kumdhalilisha kingono Tara Reade ambaye alikuwa afisa wake wa zamani, huku akiongeza kuwa kisa hicho ambacho mwathiriwa anadai kilitendeka mwaka 1993, hakikutokea.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha MSNBC, Biden amekivunja kimya chake cha mwezi mmoja kuhusu suala hilo kwa kusema kuwa hajawahi kutenda uhalifu huo.
Aidha, taarifa ya Biden imesema waliokuwa wasaidizi wake wakuu mnamo wakati kisa hicho kinadaiwa kutokea, wamekanusha kufahamu tukio hilo.
Mgombea huyo wa Democrat amesema ataiomba idara ya taifa inayohusika na kuweka rekodi kuchunguza ikiwa kuna rekodi yoyote ya malalamiko hayo.
Reade ni miongoni mwa wanawake ambao wamelalamika kwamba Biden aliwabusu na kuwashika kwa njia isiyofaa.
Joe Biden atakiwakilisha chama cha Demokratic katika mchuano wa Urais nchini Marekani Novemba Mwaka huu ambapo atachuana na Rais wa sasa Rais Donald Trump
Joe Biden atakiwakilisha chama cha Demokratic katika mchuano wa Urais nchini Marekani Novemba Mwaka huu ambapo atachuana na Rais wa sasa Rais Donald Trump