Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence anaripotiwa kwamba atakwenda karantini nyumbani kwake baada ya mshauri mmoja wa Ikulu ya White House kupimwa na kupatikana na maambukizi ya virusi vya corona.

Ikulu hiyo imekanusha taarifa hizo za vyombo vya habari na kusema kwamba makamu huyo wa rais atarudi kufanya majukumu yake hii leo.

Kulingana na serikali ya Marekani, makamu huyo wa rais amepimwa mara kadhaa ila hajapatikana na virusi hivyo vya corona.

Coronavirus latest: US Vice President Mike Pence in self-isolation ...

Huku hayo yakiarifiwa, inaripotiwa kwamba idadi ya watu waliofariki kwa virusi vya corona Marekani kwa sasa imeongezeka na inakaribia kufika 80,000. Marekani ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya vifo na maambukizi duniani kutokana na virusi vya corona.

The post Ikulu ya Marekani yakanusha makamu wa Rais kuwa na Corona appeared first on Bongo5.com.