Gavana wa Mji Mkuu wa kibiashara nchini Nigeria wa Lagos ametishia kurejesha marufuku ya shughuli za umma iwapo wakaazi wa mji huo wataendelea kupuuza masharti ya mikusanyiko yaliowekwa kupambana na virusi vya corona.
Amri ya wiki tano ya kubakia nyumbani iliondolewa mjini Lagos siku ya Jumatatu lakini tangu wakati huo makundi ya watu yanafurika kwenye masoko na mabenki licha ya kuwepo marufuku ya kuzuia mikusanyiko.
Gavana Babajide Sanwo-Olu wa mji huo amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa inakatisha tamaa kushuhudia mikusanyiko mikubwa ya watu kwenye maeneo ya mji huo inayokiuka miongozo iliyowekwa.
Olu amesema iwapo hilo litaendelea watalazimika kurejesha viuzizi vya watu kutembea kwenye mji wa Lagos ulio kitovu cha virusi vya corona nchini Nigeria. Hadi sasa taifa hilo la Afrika Magharibi limethibitisha visa 3,912 na vifo 117 vya ugonjwa wa COVID-19
The post Gavana wa Lagos, Nigeria atishia kurejesha marufuku ya shughuli za umma appeared first on Bongo5.com.