Aliyekuwa meneja wa @barakahtheprince_ @faky_junior amewashauri wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kuwa waisome na kuielewa biashara wanayoifanya kabla ya kutaka kuonekana na kujilikana.
Akiongea na Bongo5 ameongeza kuwa “Wasanii wengi wanataka kuingia kwenye muziki kwa kuhitaji umaarufuru na kutaka kuonekana ila sio waingia kwenye muziki kibiashara, Na ndio mana tutabaki kuona wasanii wale wale wakifanikiwa, Mbali na hilo wengi pia wanatakiwa wapate Elimu kuhusu Youtube jinsi inavyofanya kazi maana wengi wanaitegemea kama sehemu ya biashara yao, lakini kubwa zaidi ni kwenye mikataba yao na msanii wa Tanzania ukitaka kumchanganya muandikie mkataba kwa Kiingereza na muahidi utaenda kumshutia video mbili Afrika Kusini”
@faky_junior ameongea hayo baada ya kuthibitisha kushindwana kikazi na @barakahtheprince_ kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake.
The post Faky Junior “Tanzania muahidi msanii video Afrika kusini, Unammaliza hataki mkataba” – Video appeared first on Bongo5.com.