Viongozi walioapishwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kuanzia kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Dkt. Delphine Magere-RAS Pwani, Jacob Kingu-Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Phaustine Kasike Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi John Simbachawene Balozi wa Tanzania nchini Kenya pamoja na Brigedia General John Mbungo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.
 Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya.Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Phaustine Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020.
 Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Generali John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020.

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Viongozi mbalimbali aliowaapisha Wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020.
PICHA NA IKULU