Pesa haijifichi. Rais wa lebo ya muziki ya #WCB @diamondplatnumz anazidi kudhihirisha utajiri wake hii ni baada ya kupost picha ikimuonesha akiwa amevaa saa yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 320 za Kitanzania

Saa hiyo inafahamika kwa jina la #RichardMille na inauzwa Dola za Kimarekani 141,762 ambayo kwa Tanzania ni zaidi ya Milioni 320

Saa hii ilishawahi kumtoa nishai Mchekeshaji na mshindi wa Big Brother Afrika @idrissultan baada ya wajuzi wa mambo kumshtukia baada ya kuvaa Feki ya saa hii. Kurasa moja mtandaoni maarufu kama #FakeWatchBusta ilichapisha taarifa mnamo mwaka 2016 kuwa Mchekeshaji huyo alikuwa amevaa saa feki na kujianika nayo mtandaoni. Hii ni baada ya saa ya @idrissultan kukosa baadhi ya nakshi zinazopatikana kwenye saa hiyo ikiwa Original