Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo @jokatemwegelo amesema Hospitali Ya Wilaya Kisarawe katika kuwalinda wahudumu wa afya walio mstari wa mbele katika mapambano ya #covid19 imeanza kuzalisha mavazi maalum ya kujikinga (PPE).


Kupitia ukurasa wake wa Instagram DC Jokate ameandika:-
#Repost @jokatemwegelo with @make_repost
・・・
Hospitali Ya Wilaya Ya Kisarawe katika kuwalinda wahudumu wetu wote wa afya waliomstari wa mbele katika mapambano haya ya #covid19 tumeanza kuzalisha PPE zetu. Pamoja na hayo tulishaanza kuzalisha barakoa na vitakasa mikono vyote tayari vinapatikana kwenye famasia/pharmacy yetu, wilayani kwasasa. Naipongeza Emergency Team yetu ya Afya kwa ubunifu huu na kwa kujiongeza. ‪Kuhusiana na ubora wa vazi letu la PPE; Quality ni kama ile ya Muhimbili kwa maana ya material iliyotumika lakini kwa maana ya uimara yetu imeongezwa uimara wa ndani kuzuia isichanike/kutatuka haraka wakati wa kuitumia. ‬
@innocentbash @rc_pwani #KisaraweMpya #TanzaniaMpya

The post DC Jokate “Kisarawe tunatengeneza PPE zetu kwa ajili ya wahudumu wetu wa afya” appeared first on Bongo5.com.