Rais wa Liberia George Weah ametunga wimbo utakaotumiwa na Umoja wa Mataifa kuhamasisha watu kuhusu virusi vya corona.

Weah anatarajia kuwa watu wa taifa hilo la Afrika Magharibi lenye watu wapatao milioni 4.5 na wapenzi wa muziki barani Afrika watahamasika kwa wimbo huo wenye ujumbe wa kuhakikisha maambukizi ya virusi vya corona hayaenei zaidi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Weah kutumia kipaji chake cha kuimba. Aliwahi kutoa wimbo wa kuhamasisha wakati wa mripuko wa ugonjwa wa Ebola mnamo mwaka 2014.

Kwa mujibu wa afisi ya rais, wimbo huo kwa jina ” Tuungane kukabiliana na virusi vya corona” utakuwa ni sehemu ya awamu ya pili ya kampeni ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO inayohusu kulihamasisha bara la Afrika kuhusu hatari za virusi hivyo.

The post COVID -19: Umoja wa Mataifa kutumia wimbo wa Rais wa Liberia kuhamasisha appeared first on Bongo5.com.