Wizara ya mambo ya nje ya Colombia imetoa taarifa ikikanusha Colombia kuhusika na majaribio ya mapinduzi ya kisiasa nchini Venezuela.

 Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Bw. Nestor Reverol amesema mamluki wa Colombia walijaribu kutekeleza shughuli za kimabavu na kufanya mapinduzi kutoka pwani ya jimbo la La Guaira, kaskazini mwa nchi hiyo.

 Kikosi cha usalama cha Venezuela kimepambana na magaidi hao, na kuwaua na kuwakamata baadhi yao. 

-CRI