Msanii wa Bongo Fleva @chinbees amefungua kampuni yake itakayohusika na mambo ya Burudani the nayoitwa #BEES GANG ENTERTAINMENT.

Mbali na hilo @chinbees ameeleza kuwa ukimya wake ulisababishwa na harakati za kufungua kampuni hiyo “Nilikuwa kimya haimaanisha niliacha muziki au niliogopa, nimewasoma wasanii wanaofanya aina ya muziki ninaofanya hakuna walichofanya naona wanapiga kelele tu, Sasa nimerudi na acha niwafundishe Trap inavyotakiwa “

@chinbees ameongeza kuwa ili kuonyesha hayoaneno anayoongea ni kweli amesema kuwa muonyeshe msanii yeyote anayefanya Trap na ngoma yake ikawa kubwa zaidi ya KABABAYE au PEPETA “Mimi ndio niliwafungua wasanii Bongo na kuwaonyesha Trap ilivyo wote wakafuata, kama kuna mtu anabisha anionyeshe ngoma moja kali ya Trap kushinda KABABAYE “

The post Chin Bees afungua kampuni “Wasanii wa Trap wana muziki wa kizamani wajifunze kupitia Kababaye, Hakuna wa kushindana na mimi” – Video appeared first on Bongo5.com.