Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John  Magufuli  ameagiza vyuo vikuu vyote hapa nchini vifunguliwe kuanzia tarehe 1 mwezi wa 6 Mwaka huu sambamba na wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiandaa kwa mitihani yao.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi May 21, 2020 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni

“Kutoka na kwamba hali kwa sasa ipo vizuri na corona inapungua, tumeamua vyuo vyote vifunguliwe June 01 mwaka huu, Form six ambao wanajiandaa na mitihani yao na wao watarudi shuleni June 01, 2020

“Kwa Shule nyingine za Sekondari na Shule za Msingi tuzipe muda kidogo kwasababu Vyuo wanajitambua tofauti na Shule za Msingi huko kuna Watoto hasa darasa la kwanza kwahiyo huko napo tujipe muda kidogo

Aidha, Rais Magufuli  amesema Michezo pia itaanza tarehe 01 mwezi wa sita....“Katika trend tuliyoiona sina uhakika kama kuna mwanamichezo aliyekufa kwa corona na michezo ipo mingi kila mmoja ana michezo yake, lakini michezo inasaidia kupambana, kwahiyo kuanzia June 01,2020 michezo irudi kama kawaida.

"Taratibu za kushangilia na kuangalia Wizara ya Afya na inayohusika na Michezo watapanga ili utaratibu wa social distance ukaendelea kuwepo." Amesema Rais Magufuli