Ben Ishabakaki ambaye ni Mwanasheria wa msanii Idriss Sultan amerhibitisha kukatwa kwa mteja wake leo kwenye kituo cha polisi cha Oyesterbay jijini Dar es salaaam

Ishabakaki ameuambia mtandao wa Jamii forums kuwa mteja wake alikamatwa leo alipokwenda kuitikia wito wa polisi kituoni hapo kutokana na makosa ya mtandao

Ikumbukwe kuwa Oktoba 2019, Idriss alikamatwa kwa kuhariri picha ya Rais Magufuli na alihojiwa kwa saa 5 katika Kituo cha Polisi Central, kisha kuachiwa kwa dhamana

Aidha, Idris aliyewahi kushinda tuzo ya Big Brother Africa mwaka 2014, Machi mwaka huu (2020) alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu kwa kuweka maudhui mtandaoni bila leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)