Brazil imerekodi vifo vipya 615, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuripotiwa kwa siku moja. Waziri wa Afya, Nelson Teich amesema Serikali inaweza kuanza kuweka masharti ya kutotoka ndani katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Msemaji wa Rais Jair Bolsonaro, Otavio Rego Barros (59) amethibitishwa kupata #COVID19 na mpaka sasa, watumishi wa juu zaidi ya 20 wa Rais huyo wamepata maambukizi akiwemo Waziri wa Usalama wa Taifa, Augusto Heleno

Rais Bolsonaro amesema vipimo vinaonesha hana maambukizi na amekuwa akihamasisha wananchi kuendelea kufanya kazi kama kawaida licha ya ongezeko la maambukizi na vifo

Hadi kufikia leo, Brazil imerekodi visa 126,611 na vifo 8,588 huku wagonjwa waliopona Virusi vya Corona wakiwa 51,370

The post Brazil watangaza vifo vipya 615, watumishi 20 wa ngazi za juu wakutwa na maambukizi appeared first on Bongo5.com.