Beki wa Klabu Bursa Yildirim Spor, Cevher Tokts raia wa Uturuki amekiri kumuua mtoto wake kwa kuwa alikuwa hampendi na kujisalimisha polisi.

Tukio hilo, lilitokea Aprili 23, mwaka huu ambapo beki huyo alimpeleka mtoto wake huyo wa miaka mitano hospitali baada ya kuonyesha dalili za virusi vya corona. –

Lakini baadaye, mchezaji huyo aliwaambia wauguzi kuwa mtoto wake huyo wa kiume alikuwa na tatizo la kushindwa kupumua hivyo alipelekwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na kisha kufariki.

Hata hivyo baada ya siku kaadha, mchezaji huyo alijipeleka polisi mwenyewe na kukiri amemua mtoto huyo kwa sababu alikuwa hampendi.

Mchezaji huyo alisema: “Mtoto alikuwa amelala nikachukua mto na kuweka kichwani na kumfumba mdomo kwa dakika 15,” alikiri mwenyewe mbele ya polisi na aliendelea kusema: “Nilikuwa simpendi tangu alipozaliwa na sijui kwa nini na ndiyo maana niliamua kumuua sababu nilikuwa simtaki na sina tatizo lolote la akili.

”Hata hivyo, Polisi wa Uturuki bado wanamshikilia mchezaji huyo na huenda akafungwa maisha.

 

The post Beki wa klabu ya Bursaspor ya Uturuki amuua mtoto wake wa miaka 5, Asema “Nilikuwa simpendi” appeared first on Bongo5.com.