Mabingwa wateizi wa ligi ya Bundesliga, Bayern Munich wamepanga kutoa keki katika jumla ya nyumba 80 ambazo zinawaangalia (kulea) wazee katika jimbo la Bavaria kama hatua ya kuwatia moyo vikongwe na watumishi wao na kuwahakikishia kwamba jamii iko pamoja nao wakati huu wa janga la corona.

FC Bayern sends signal of solidarity with the elderly and nursing ...

Bayern imesema katika taarifa yake ya hapo jana siku ya Ijumaa kwamba kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya jimbo la Bavaria 10 kati ya keki maarufu kwa jina Sachertorten zitakwenda kwa kila nyumba ya wazee wiki ijayo.

“Wazee ndio watu wanaoteseka zaidi kutokana na corona, kisaikolojia pia. Hasa katika kipindi hiki ambacho watu hawaruhusiwi kutembeleana. Tunataka kuwaambia kwa kutumia ukarimu huu, hamko peke yenu,” alisema mwenyekiti wa klabu ya Bayern, Karl-Heinz Rummenigge.

FC Bayern sends signal of solidarity with the elderly and nursing ...

“Watumishi wa wazee hufanikisha mambo makubwa kwa jamii kila siku. Kazi hii inahitaji nguvu nyingi na kujitolea sana. Lazima wawe na sifa nyingi kitaaluma na hata kuwa na huruma,” aliongeza kusema.

Ligi ya Bundesliga ilisitishwa katikati ya mwezi Machi kwa sababu ya janga la virusi vya corona. Klabu zina matumaini ya kuukamilisha msimu kuanzia mwezi Mei kuendelea.

The post Bayern Munich kutoa keki kwa Wazee appeared first on Bongo5.com.