Hertha, Berliner Sport-Club (Hertha BSC) ya nchini Ujerumani imemsimamisha mshambuliaji wake Salomon Kalou baada ya kutuma video kwa mtandao wa Facebook iliyomuonesha yeye na wachezaji wenzake wakisalimiana kwa mikono na kuvunja masharti ya kudhibiti COVID-19.
Klabu ya Hertha Berlin imesema Jumanne hii katika taarifa kwamba “hii ni tabia ya mchezaji mmoja” na kukanusha madai kwamba kikosi kizima hakizingatii utaratibu wa kutokaribiana na sheria za usafi kwa uzito unaotakiwa.
Mchezaji huyo wa Ivory Coast ameomba radhi kwa tabia yake ambayo kitengo cha ligi kinachopanga ratiba ya mechi za Bundesliga, DFL, kiliileza kwenye mtandao wa Twitter kuwa “isiyokubalika kabisa”.
Hertha, ambayo imesema video hiyo ilitayarishwa baada ya kikosi kizima kutopatikana na maambukizo ya virusi vya corona, ilikiri kwamba katika sehemu moja video hiyo inawaonesha wachezaji wakisalimiana kwa mikono huku Kalou pia akionekana akitatiza upimaji wa kitabibu wa wachezaji wenzake.
“Video ya Salomon Kalou kutoka chumba cha kubadilishia nguo ilikiuka sheria ya msingi wa timu na kuonesha tabia isiyofaa kwa hali iliyopo na haiendani na sheria za maadili za klabu,” ilisema taarifa.
“Hertha BSC kwa hiyo imeamua kumsimamisha mara moja kutoka mazoezi na kucheza.”
Taarifa iliongeza: “Salomon Kalou alishawishiwa na matokoe ya vipimo kuwasalimia wachezaji wenzake katika chumba cha kubadilishia nguo, wakati mwingine kwa kuwasalimia kwa mkono, kinyume na matangazo ya wazi ya afisa wa usafi.”
Meneja wa Hertha, Michael Preetz, amesema Kalou ameisababishia klabu hiyo “ameiharibia sifa yake” na “kutoa taswira kwamba wachezaji hawalichukulii suala la corona kwa uzito.”
Preetz alisema klabu hiyo ilielezea kinagaubaga suala la usafi na sheria ya kutojongeleana kwa wafanyakazi wake wote.
Kalou, mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea, Lille na Feyenoord ambaye ameichezea Ivory Coast mechi 90, ameombadha radhi.
“Sikufikiria kwa kweli na nilifurahi kwamba majibu ya vipimo vyetu hayakuonesha tumeambukizwa,” alisema, akiongeza kuwa ana wasiwasi mkubwa sana kuhusu hali ya janga la corona barani Afrika.
“Ningependa pia kuomba msamaha kwa wale walioonekana kwenye video ambao hawakujua nilikuwa nikionyesha video mubasahra na ambao sikutaka kuwaweka katika hali kama ile.”
The post Asimamishwa ndani ya klabu baada ya kuonekana akipeana mikono na wachezaji wenzake appeared first on Bongo5.com.