Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa Kylian Mbappe ndiye mchezaji pekee ambaye anaamini kwa upande wake anaweza kuja kuchukua nafasi ya miamba hii miwili ya soka duniani Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Licha ya kuwepo kwa mitazamo tofauti juu ya nani atakayekuwa na uwezo wa kuja kuchukua nafasi ya nyota hawa wawili wanaosumbua dunia katika ulimwengu wa soka kwa sasa, huku wengine wakimuhusisha mchezaji wa klabu ya PSG, Neymar  kwa upande wake Wenger anaamini kijana huyo ambaye pia ni mshindi wa kombe la dunia mwaka 2018, Kylian Mbappe ndiye mwenye nafasi kubwa.

Wenger anaamini kuwa Neymar atakuja kumpa changamoto Mbappe hapo baadaye kwakuwa ufalme wa Messi na Ronaldo unaelekea kufikia kikomo kutokana umri wao kusonga licha ya kuwa bado wanavitu vya tofauti.

“Lionel Messi, hatukuwahi kuona mchezaji kama yeye hakika, mbunifu hata akiwa katika mazingira magumu,” bosi huyo wazamani wa Arsenal amekiambia chombo cha habari cha talkSPORT.

Wenger ameongeza “Hawa wachezaji kwa sasa mwisho wao unakaribia, Ronaldo na Messi. Kwa sasa tunafikiria kizazi kijacho, na kizazi hicho kijacho pengine ni kutokea Ufaransa, wakati huo atakayewaongoza atakuwa Mbappe.”

The post Arsene Wenger amtaja mrithi wa Messi na Ronaldo, atokea taifa hili appeared first on Bongo5.com.