Msanii mpya wa WCB, Zuchu ametoa kauli yake ya kwanza ikiwa ni wiki moja toka atambulishwe rasmi WCB.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo Wana, amedai angejua kama alikuwa anaandaliwa maisha yake mazuri na label hiyo basi asingelalamika wala kulia. “Eh Mungu,😢, naziona neema zako, laiti ningejua kama kubiriwa kote naandaliwa kwa hili nisingefungua mdomo kulalamika wala kutoa machozi,” alisema Zuchu kupitia ujumbe aliouandika Instagram.

Aliongeza,”Kweli wakati wa Mungu ndio wakati sahihi eti nyimbo yangu iko namba moja trending boomplay mimi?. Alhamdulillah, shukrani zangu za dhati kwa Diamond na uongozi wa WCB.” Zuchu aliwahi kushiriki shindano ya kusaka vipaji vya muziki  barani Afrika mwaka 2016 liitwalo  Tecno Own The Stage ambalo pia msanii Faustina Charles maarufu Nandy naye alishiriki na kupata Sh36 milioni baada ya kuwa mshindi wa  pili.

Baadhi ya nyimbo ambazo Zuchu ameshirikishwa kabla ya kusainiwa WBC ni pamoja na ule wa Superwoman uliowahusisha wasanii mbalimbali wa kike nchini Tanzania ulioimbwa maalum kwa ajili ya kusherehekea siku ya wanawake duniani.

 

The post Zuchu: Ningejua mambo yako hivi WCB nisingelalamika wala kulia (Video) appeared first on Bongo5.com.