Wizara ya Afya Zanzibar imetangaza Waathirika wapya 6 na kufanya idadi ya Waathirika visiwani humo kufikia 24 kutoka 18 waliotangazwa Aprili 15, 2020. Wagonjwa wote wamelazwa katika vituo maalum vya matibabu

Mmoja ni Mwanaume, Mtanzania (30), mwingine ni Mwanaume, Mtanzania (27), wa tatu ni Mwanaume pia Mtanzania (28), wa nne ni Mwanaume, Mtanzania (23), mwingine ni Mwanamke, Mtanzania (58) na wa mwisho ni Mwanaume, Mtanzania (55)

Aidha, Wizara imesema wote hawana historia ya kusafiri nje ya nchi siku za hivi karibuni huku ikiwaomba Wananchi wenye dalili za homa kali, kukohoa na kupiga chafya kupiga simu namba 190

Wizara imewataka Wananchi wanaofiwa kuchukua tahadhari kwa namna ya kuwashughulikia, kuwakafini na kuwazika ndugu zao na kuwashauri washirikiane na Wataalamu wa Afya kwa kupata miongozo stahiki

The post Zanzibar watangaza wagonjwa wapya 6 wa corona, waathirika wafikia 24 appeared first on Bongo5.com.