Kuanzia New Zealand hadi Ujerumani,Taiwan au Norway, baadhi ya nchi zinazoongozwa na wanawake zimeonyesha kuwa na idadi ndogo ya vifo kwasababu ya ugojwa wa Covid-19.

Na wanasiasa wa nchi hizo wanasifiwa na vyombo vya habari kwa mitazamo yao juu ya ugonjwa huo pamoja na hatua walizozianzisha kukabiliana na janga hili la afya.

Makala ya hivi karibuni katika jarida la Forbes liliwaonesha kama mfano wa kuigwa katika uongozi.

“Wanawake wamejitokeza na kuonyesha dunia vile wanavyoweza kuwa kupambana na kile ambcho kimejitokeza kuandama familia zetu”, jariba la Forbes liliandika.

Wachambuzi nao wakiongeza kuwa wale wanaopita mtihani huu wa Covid-19 kwa kiasi kikubwa ni wanawake licha ya kwamba wale walio katika ngazi ya uongozi kama wakuu wa nchi kote duniani ni asilimia 7 pekee.

Je ni kipi kinachofanya viongozi wanawake kufanikiwa katika kukabiliana na janga la corona?

Hatua za mapema

Waziri Mkuu wa Iceland Katrín Jakobsdóttir amegeukia upimaji wa virusi vya corona wa halaiki.

Licha ya kwamba ni nchi yenye idadi ndogo ya watu ya 360,00, imekataa kulegeza kamba katika hatua za kupambana na Covid-19 kama vile kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya 20 au zaidi iliyochukuliwa mwishoni mwa Januari, kabla hata haijarekodi hata kisa kimoja cha ugonjwa huo.

These female leaders have acted quickly and based on scientific considerations
Image captionWanawake viongozi ambao wamechukua hatua za haraka kukabiliana na ugonjwa wa corona

Kufikia Aprili 20, watu 9 walikuwa wamekufa kwasababu ya Covid-19.

Huko Taiwan, ambayo ni sehemu ya China, Rais Tsai Ing-wen alianzisha kituo cha kudhibiti janga hilo na kuchukua hatua za kudhiiti na kufuatiliana wale walioambukizwa.

Taiwan pia mara moja ilianza uzalishaji wa vifaa vyake vya kujilinda kama vile barakoa. Hadi kufikia sasa imerekodi vifo 6 pekee miongoni mwa raia milioni 24 wa nchi hiyo.

Wakati huohuo, New Zealand, Waziri Mkuu Jacinda Ardern amechukua moja ya hatua kali zaidi ya kukabiliana na Covid-19. Badala ya kupunguza idadi ya visa vya maambukizi,kama vile ilivyodhihirika kwa nchi zingine, mbinu aliyotumia Bi. Ardern ni ya kuangamiza maambukizi yote.

Nchini humo kulitangazwa amri ya kusalia ndani vifo vilipofikia 6 pekee na kufikia Aprili 20, kwa ujumla vilikuwa vimefikia 12.

Taiwan President Tsai Ing-wen (C), seen wearing a face mask amid the COVID-19 coronavirus pandemic alongside soldiers and officialsHaki miliki ya pichaSAM YEH/AFP
Image captionRais wa Taiwan Tsai Ing-wen (katikati), akionekana akiwa amevaa barakoa pamoja na wanajeshi na maafisa wengine

Lakini mbali na kwamba wanawake wanafanya vizuri katika kupambana na covi-19, nchi hizi ambazo zinachukuliwa kuendelea vizuri, zina wengine yanayofanana:

Hizi zote ni nci zenye uchumi ulioendelea, na mfumo wa ustawi wa jamii na mara nyingi huwa imeimarika kwa maendeleo ya jamii.

Kama iayojitikeza ni nchi zenye mifumo iliyoimarika ya afya yenye uwezo wa kukabiliana na hali ya dharura.

Kwahiyo, hilo linahusu viongozi wenyewe – au pengine pia inaangazia vile inavyomaanisha kuwa na kiongozi mwanamke katika nchi?

A woman, wearing a face mask, walks past a sign guiding people to the entrance of a corona testing station at the Vivantes Wenckebach hospital in BerlinHaki miliki ya pichaODD ANDERSEN/AFP
Image captionKituo cha kupima corona katika hospitali ya Berlin hospital. Kwa mkakati wa Angela Merkel upimaji ndo ulikuwa uti wa kukabiliana na janga la corona

Bila shaka inahusiana na Uanuai

Kulingana na waangalizi, vile wanawake hao wanavyojitokeza na kufanya kampeni zao pia ni jambo la msingi.

“Sidhani kwamba wanawake mtindo mmoja wa uongozi ambao ni tofauti na wanaume. Lakini wanawake wanapokuwa katika nafasi za uongozi, hilo linachangia mbinu tofauti katika ufanyaji wa mamuuzi,” amesema Daktari Geeta Rao Gupta, mkurugenzi wa Programu ya 3D kwa wasichana na wanawake na maafisa waandamizi katika wakfu wa Umoja wa Mataifa.

“Kunafanya kuwe na maamuzi mazuri kwasababu una maoni ya wanaume na wanawake,” ameiambia BBC.

Ni tofauti kabisa na wale walioegemea siasa kwa baadhi ya viongozi wanaume kama Rais wa Marekani na Donald Trump na Brazil Jair Bolsonaro.

President Jair Bolsonaro shakes hand with a supporter on 15 March, amidst the Covid-19 outbreak in Brazil, 15 MarchHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Brazil Jair Bolsonaro ameita ugonjwa wa Covid-19 “mafua tu” na kukiuka mara kadhaa kanuni ya kutokaribiana

Rosie Campbell, mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake duniani katika chuo kikuu cha Uongozi wa wanawake cha King’s London, anakiri kuwa mtindo wa uongozi sio sawa kwa wanaume na wanawake.

“Lakini kwa namna tunavyojadiliana, inakubalika kwa wanawake kuwa wenye huruma na ushirikiano zaidi. Na pia kuwa wanaume zaidi ambao pia wapo kwenye kundi hili watu binafsi, na ushindani wa kupitiliza”, Campbell amesema.

Anaamini kuwa sifa kama hizo kwenye uongozi wa wanaume matatizo kwa misingi ya kisiasa”.

Tatizo la siasa za mfumo dume

Viongozi wanaotegemea mambo mashuhuri wanategemea sulusho rahishi ili kupata uungwaji mkono, ameiambia BBC na mara nyingi hili limeathirimbinu zao za kukabilia janga.

Viongozi wa kisiasa nchini Marekani, Brazil, Israel na Hungary na nchi zingine kidogo mara kadhaa zimejaribu kutupia lawama sababu zengine kwasababu ya makosa yao kama vile kulaumu raia wa kigeni kuwa cha ugonjwa huo kwa nchi husika.

“Trump na Bolsonaro wameamua kuchukua mkondo wa kujionesha kwamba wao ni waumme. Sio kwamba ni lazima wao kuonesha tabia kama hizo lakini wameamua kufanya hivyo,” Profesa Campbell anasema.

“Ni mara chache sana utaona wanawake wakifuata mkondo wa wanaotaka kuwa maarufu. Ingawa kuna wale waliotofauti kama vile Marine Le Pen [nchini Ufaransa].

“Lakini kwa ujumla, lakini hilo linahusishwa zaidi na maamuzi ya mtu binafsi.”

Barabara ya Austurstraeti eneo la Reykjavik, Iceland Aprili 3, 2020.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIceland ilianza kupima watu kwa halaiki pamoja na kutoa marufuku ya mapema ya didhi ya mikusanyiko ya watu zaidi ya 20.

Watu wa wanavyoshughulikia janga la Covid-19 bila shaka kunatofautiana, pengine kwa kiasi fulani hilo linachangiwa na uwezo wa nchi kijamii na kiuchumi na raslimali zilizopo – ambapo huenda jinsia isiwe na mchango wowote kwa hilo.

Hivyobasi, viongozi wanaume ambao sio miongoni mwa wenye mitazamo iliyoelezwa na Profesa Campbell pia nao wanashuhudia idadi ndogo ya vifo katika nchi zao.

Korea Kusini, jinsi rais Moon Jae-in alivyokabiliana na janga la corona kumekuwa nguzo muhimu kulikochangia ushindi wake wa ubunge uliofanyika Aprili 15.

Na Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis pia nae amesifiwa kwa kufanikiwa kukabiliana na janga hilo na idadi ya vifo kuwa chini (114) kufikia Aprili 20, kwa nchi yenye idadi ya watu karibia milioni 11.

Ukilinganisha kwa Italia yenye idadi ya watu milioni 60, imekuwa na vifo 22,000.

Ugiriki inakanikiwa katika vita dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kutoa kipaumbele kwa ushauri wa kisayansi na pia ilianza kutekeleza hatua ya kutokaribiana mapema – kabla ya kurekodi kisa chake cha kwanza.

Healthcare workers wearing face masksHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWanawake ni asilimia 70za wahudumu wa afya kote duniani lakini bado wako nyumba katika nafasi za uongozi

Na pia baadhi ya nchi zinazoongozw na wanawake zinakumbana na changamoto kubwa kuzuia virusi hivyo vinavyosambaa kwa haraka.

Kwa mfano, Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina amefanikiwa kudhibiti maambukizi katika moja ya nchi zenye idadi kubwa ya watu.

Lakini pia kuna wasiwasi wa upungufu wa vifaa vya kupimia na wafanyakazi wa wizara ya afya Bangladeshi wanasema kwamba wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa virusi hivyo kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujikinga.

Maamuzi magumu

Ili kuzuia Covid-19 , viongozi wamejipata wakifanya maamuzi magumu kama vile kufunga shughuli zote za kiuchumi katika nyakati za mwanzo za maambukizi.

Lakini maamuzi kama hayo, yana gharama kubwa kisiasa katika kipindi cha muda mfupi, tofauti na vile wanavyotaka viongozi wanaotegema umaarufu”, Profesa Campbell amesema.

Angela Merkel wa Ujerumani alikubali mara moja kwamba ugonjwa wa Covid 19 ni tishio kubwa.

Nchi yake imekuwa na vifaa vingi vya kufanyia majaribio, kutafuta walioambukizwa na kuwatenga. Zaidi ya watu 4,600 wamekufa kwa virusi vya corona huko Ujerumani ambayo idadi ya watu milioni 83.

Mbinu zilizotumika na Norway na Denmark zenye waziri wakuu wanawake, pia nazo zimefanya vizuri.

The Prime Ministers of Norway, Erna Soldberg (L), and Denmark, Mette Frederiksen
Image captionViongozi wa Norway na Denmark wamefanya mkutano na wanahbari kuzungumzia masuala kadhaa ya watoto

Kiongozi wa Norway, Erna Solberg, na mwenzake wa Denmark, Mette Frederiksen, amefanya mkutano na wanahabari kuzungumzia suala la watoto ambapo hakuna mtu mkubwa aliyeruhusiwa kuingia ndani.

Maamuzi mazuri

Wanawake ni asilimia 70 ya wahudumu wote wa afya duniani, ilihali, 2018 ni 10 pekee kati ya 153 waliochaguliwa kuchukua nafasi za uongozi, kulingana na shirika la kimataifa la mabunge ya kitaifa.

Ni robo kutoka nchi washirika ambao ni wanawake.

Healthcare workers wearing face masksHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWanawake ni asilimia 70za wahudumu wa afya kote duniani lakini bado wako nyumba katika nafasi za uongozi

Daktari Gupta ambaye pia ni mwenyekiti wa ushauri wa bodi ya afya ya wanawake, wakfu wa Bill na Melinda Gates unaolenga kuongeza viongozi wanawake katika sekta ya afya unatoa wito wanawake wengi zaidi wajumuishwe kwenye nafasi za uongozi.

Anasema kwamba hilo litasaidia kuimarisha meza ya maamuzi.

“Kutakuwa ba maamuzi yenye uhusiano na nyanja zote za jamii, sio tu baadhi.

“Kwasababu kama wanawake, viongozi wanawake wanatajriba ya kushiriki majukumu mbalimbali katika jamii. Na hivyobasi, mitazamo na maamuzi yao huenda yakaathirika.”

Daktari Gupta ameonya kwamba kuhusu athari mbalimbali za kiuchumi na kijamii kutokana na janga la Corona kwa wanaume na wanawake: dhulma za ndani ya nyumba zimeongezeka na hatari ya kuongezeka kwa umaskini.

The post Yaelezwa mataifa yanayoongozwa na viongozi wanawake, Yafanya vizuri kwenye mapambano dhidi ya Corona appeared first on Bongo5.com.