Uingereza inaanza majaribio ya kutumia damu ya waliopona virusi vya corona kuwatibu wagonjwa walio na maambukizi hayo ambao wapo hospitali.

Taasisi ya damu na upandikizaji ya Uingereza inawataka watu waliopona homa ya mapafu, covid-19 kuchangia damu ili waweze kutathimini tiba hii iliyo kwenye majaribio.

Matumaini ni kwamba molekyuli walizozitengeneza zitasaidia kupambana na virusi vilivyo kwa wengine.

Marekani tayari imeanza mradi mkubwa wa utafiti huu, ikihusisha hospitali 1,500.

Mtu anapokuwa na virusi vya corona, mfumo wa kinga hutengeneza molekyuli, ambazo huvishambulia virusi.

Kwa kipindi fulani molekyuli hizi zinaweza kupatikana kwenye plazma, sehemu ya majimaji ya damu.

Taasisi ya damu na upandikizaji sasa inawasiliana watu waliopona Covid-19 kuona kama plazma zao zinaweza kutolewa na kupewa wagonjwa wengine wanaoumwa ugonjwa huo.

Taarifa ya taasisi hiyo imesema: ”tunatafakari uwezekano kwamba hii itatumika awali kama tiba ya Covid-19. ”Ikiwa itaidhinishwa,majaribio yatafanyika kuchunguza kama plazma hizo zitasaidia kuongeza kasi yakuimarisha afya ya mgonjwa aweze kupona haraka.

”Kila majaribio yanapaswa kufuata mchakato wa kuidhinishwa ili kuwalinda wagonjwa na kuhakikisha matokeo ya uhakika yanapatikana. Tunafanya kazi kwa ukaribu na serikali na vyombo vyote vinavyohusika kupitia mchakato wa kupata idhini haraka iwezekanavyo.”

Makundi mengine wanafanya hili?

Makundi kadhaa nchini Uingereza yamekuwa yakitazamia kutumia plazma ya damu.

Chuo cha kitabibu katika hospitali ya Wales, Cardiff ilitangaza wiki hii kuwa ilitaka kufanyia majaribio teknolojia hii.

Coronavirus

Profesa Sir Robert Lechler, rais wa shule ya sayansi ya tiba na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la King’s Health pia ana matumaini kufanya jaribio jingine dogo.

Anataka kutumia plazma kwa wagonjwa walio mahuti ambao hawana namna nyingine ya kupata tiba, wakati ambao jaribio kubwa linaendelea nchini humo.

Alisema: ”Ningesikitishwa sana kama tusingeweza kuwaona baadhi ya wagonjwa wakipewa aina hii ya tiba ndani ya majuma kadhaa. Tuwe na matumaini kuwa majaribio yanayofanywa na benki ya kitaifa ya damu yaanze haraka sana.”

Amesema Uingereza imechukua hatua taratibu mno kujaribu tiba hii.

”Ninafikiri kuna namna tofauti ya janga hili tunaweza kutazama na kulisema, ninashangaa kwa nini hatukuharakisha. Ninafikiri suala hili linaweza kuwa moja ya masuala ya kushughulikiwa haraka”.

Hali ipoje kwengineko duniani?

Duniani kote,majaribio yanaendelea wakitazamia kutumia plazma.

Katika kipindi cha majuma matatu pekee, wanasayansi nchini Marekani wamejiunga kwa ajili ya mradi wa kitaifa na karibu wagonjwa 600 wametibiwa mpaka sasa.

Profesa Michael Joyner kutoka hospitali ya Mayo, anaongoza kazi hiyo.

Woman coughing

Anasema: ”Kitu tulichojifunza katika juma la kwanza la kazi hii ni kuwa kuwa hakuna tahadhari za kiusalama zilizojitokeza na kuwa tiba hii haijaonekana kuonesha athari ambazo hatukuzitarajia.

”Kuna mengi tussiyoyaelewa kuhusu plazma. Tutajifunza kuhusu plazma nini, vitu gani vinaiunda, na masuala mengine kuihusu kadiri muda unavyoendelea.

Ni kwa namna gani njia hii ilisaidia kutibu magonjwa mengine awali?

Kutumia damu ya watu waliopona si tiba mpya katika masuala ya kitabibu. Ilishawahi kutumika kabla njia hii zaidi ya miaka 100 iliyopita wakati wa ugonjwa wa mafua ya Uhispania, na zaidi hivi karibuni Ebola na Sars.

Mpaka sasa, tafiti ndogo ndogo zimetazama ufanisi wake, na kuna kazi kubwa katika utafiti inayopaswa kufanywa kutazama namna gani ufanisi huu utaonekana dhidi ya virusi vya corona.

Lakini nchini Marekani, wanasema hawana upungufu wa watu wanaotaka kusaidia.

”Tuna mamia kwa mamia ya wachangiaji na tumeweza kukusanya damu kiasi cha uniti 1,000 tayari. Inatia moyo kweli kuona kuwa watu walioathirika wanafikiria namna ya kuwasaidia wengine”.

Hata hivyo wanasayansi wanasema plazma haiwezi kufanya mazingaombwe.

Lakini wakati hakuna namna nyingi za kutibu virusi , kuna tumaini njia hii itasaidia mpaka pale chanjo itakapopatikana.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

The post Yaelezwa damu ya watu waliopona Corona inaweza kuwa tiba ya ugonjwa huo, Utafiti waendelea appeared first on Bongo5.com.