Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia CHADEMA Wilfred Lwakatare, jana Aprili 14, 2020, amesema kuwa kwa sasa atapumzika katika siasa ambazo amezitumikia kwa miaka mingi na kwamba hana deni na mtu yeyote hata wale ambao aliwahi kushindana nao walikwishamalizana.

Lwakatare anaungana na Mbunge wa Kuteuliwa, Alhaj Abdallah Bulembo na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) ambao wametangaza kutogombea tena ubunge.

Mbunge huyo anakuwa ameongoza jimbo hilo kwa miaka kumi.

Akichangia jana mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2020-2021, Lwakatare alilishukuru Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Bukoba Mjini kwa kufanya nao kazi vizuri.