Mkuu wa shirika la Afya duniani WHO ametaka kuwepo kwa umoja huku shirika hilo likiendelea kushambuliwa na rais Donald Trump.

Akizungfumza siku ya Jumatano, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus alitetea kazi ya shirika hilo na kutoa wito wa kusitishwa kwa siasa katika mlipuko wa virusi vya corona.

Bwana Trump alionya kwamba atafikiria kusitisha ufadhili dhidi ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

Rais huyo alilishutumu shirika hiko kwa kuipendelea China na kudai kwamba walilisaidia sana taifa hilo.

Lakini Dkt Tedros amepinga matamshi hayo akisisitiza: ‘Tunasaidia kila taifa ,hatuna upendeleo wowote’.

Baada kulishutumu shirika la Afya duniani siku ya Jumanne, rais Trump aliimarisha upya ukosoaji wake katika mkutano na wanahabri siku ya Jumatano , akisema kwamba shirika hilo linapatia kipaumbele maswala yake muhimu.

Amesema kwamba Marekani itafanya utafiti kuamua iwapo itaenedelea kutoa ufadhili wake.

Pia akijibu maswali katika mkutano huo na vyombo vya habari siku ya Jumatano, waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba utawala wa Trump utaangazia upya ufadhili kwa shirika hilo.

”Mashirika lazima yafanye kazi. lazima kazi zao zionyesha matunda”, alisema bwana Pompeo.

Kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Covid-19 kilitangazwa mjini Wuhan nchini China mnamo mwezi Disemba.

Wuhan imekamilisha agizo la kujitenga kwa wiki 11.

Mshauri Mkuu wa WHO awali alikuwa amesema kwamba ushirikiano wao wa karibu na China ulikuwa wa kufana katika kuelewa ugonjwa huo katika hatua zake za kwanza.

Shambulio la Bwana Trump dhidi ya WHO linajiri wakati ambapo imekuwa ikiukosoa utawala wake kwa jinsi unavyolichukulia janga hilo nchini Marekani.

Je Mkuu huyo wa WHO alisema nini?

Kwa mujibu wa BBC, Dkt Tedros amesema “Tafadhali Umoja katika ngazi za kitaifa , tusitumie Covid kisiasa”, Dkt. Tedros alisema siku ya Jumatano.

”Tuwe na uaminifu na umoja . Na uongozi wa uaminifu kutoka Marekani na China”.

”Vitu muhimu vipewe kipaombele na tafadhalini wekeni siasa karantini”, aliomba katika matamshi yalioonekana yakimjibu bwana Trump.

Siku ya Jumanne, rais Trump alikuwa amesema kwamba WHO lilionekana kupendelea China.

“Walisema ni makosa. hawakuelewa tulichomaanisha, ” alisema. “na tutasitisha fedha zetu tunazolipatia WHO. Tutasitisha kabisa na halafu tutaona”.

Marekani ni mojawapo ya wafadhili wakuu wa kujitolea huku data ya WHO ikionyesha kwamba wanafadhili asilimia 15 ya jumla ya bajeti yote ya shirika hilo.Rais Donald Trump wa Marekani amelikosoa WHO

Rais Donald Trump wa Marekani amelikosoa WHO

Siku ya Jumatano bwana Tedros alipuuzilia mbali madai hayo ya vitisho vya kifedha akisema kwamba anaamini kwamba ufadhili wa Marekani utaendelea.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres mapema alikuwa amelitetea shirika hilo.

Alitaja mlipuko wa virusi hivyo vya corona kama usio wa kawaida na kusema kwamba uchunguzi wowote kuhusu jinsi ulivyoangaziwa ni suala la siku zijazo.

”Wakati huu ni wakati wa Umoja , kwa jamaii ya kimataifa kufanya kazi kwa umoja kuzuia kuenea kwa viruis hivi na madhara yake” ,alisema.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia aliliunga mkono shirika hilo alipompigia simu Tedros siku ya Jumatano.

Alisisitiza uaminifu na kuiunga mkono taasisi hiyo na kupinga hatua ya kuingizwa katika vita vya kisiasa kati ya China na Marekani, alisema afisa mmoja aliyekuwa akiongea na shirika la habari la Reuters.

The post WHO yataka siasa isihushishwe katika Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.