Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini kenya, imefikia 396  baada ya wengine 12 kuongezeka leo April 30, 2020

Wizara ya afya nchini humo  imesema kwamba kati hao 12 walioambukizwa, 7 wanatoka Mombasa, 3 Nairobi, Kitui 1 na Wajir 1.

Kwa saa 24 zilizopita, wagonjwa 15 wamepona ikiwa ndio idadi ya juu tangu kutangazwa kwa virusi hivi nchini mno huku wale waliopona wakifikia 144 kwa ujumla.
 
Aidha wawili wamethibitishwa kufariki na kufikisha idadi hiyo kuwa 17.