Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, hadi Aprili 21, 2020 jumla ya Wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na Virusi vya Corona. Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki

Mara ya mwisho Waziri wa Afya  Ummy Mwalimu alitoa taarifa kuwa jumla ya visa vya wagonjwa wa Corona  ilikuwa 254 baada ya Wagonjwa 84 kuongezeka

Aidha, Waziri Mkuu amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na Wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1733 hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284)

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumatano April 22, 2020  akiwa kwenye Maombezi ya kuombea Taifa dhidi ya ugonjwa huu yanayofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar

==>>Msikilize hapo chini