Watu bilioni moja huenda wakaambukizwa virusi vya corona kote duniani na mambo pengine yabadilike, nchi zisizojiweza zinahitaji usaidizi wa haraka, Shirika la kutoa msaada limeonya.

Kamati ya Shirika la Kimataifa la Kutoa Misaada (IRC) limesema kwamba msaada wa kifedha na kibinadamu vinahitajika kusaidia kupunguza kasi ya usambaaji wa virusi vya corona.

Shirika hilo limesema nchi zinazokabiliwa na vita kama Afghanistan na Syria zinahitaji msaada wa dharura wa kifedha kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa corona.

“Muda uliosalia kuimarisha hali ni mchache mno,” Shirika hilo limeonya.

Kumekuwa na zaidi ya watu milioni 3 walioambukizwa ugonjwa wa Covid-19 kote duniani huku zaidi ya vifo 200,000 vikithibitishwa, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Marekani.

Ripoti ya shirika hilo, ambayo inazingatia data za Shirika la Afya Duniani (WHO) na chuo cha Imperial College London, ilikadiria kwamba kunaweza kuwa na maambukizi kati ya milioni 500 na bilioni 1 kote duniani.

Pia imesema kwamba huenda idadi ya vifo ikawa ni milioni 3 katika nchi zinazokumbwa na migogoro na zisizokuwa na uthabiti.

“Idadi hiyo inastahili kutufungua macho,” amesema mkuu wa shirika la IRC, David Miliband.

“Maafa ya janga hili bado hayajashuhudiwa sana katika nchi zilizoathirika na vita,” ameongeza. “Cha msingi sasa ni kwa wafadhili kutenga pesa kwa nchi zinazokumbwa na vita.

“Serikali zinastahili kushirikiana kuondoa kizuizi chochote dhidi ya msaada wa kibinadamu.”

data kwa kina

Teremsha jedwali kuona data zaidi
vifo
Idadi ya walioambukizwa
Marekani 57,171 1,000,900
Italia 27,359 201,505
Uhispania 23,822 232,128
France 23,293 128,339
Uingereza 21,678 161,145
Belgium 7,331 47,334
Ujerumani 6,174 159,137
Iran 5,877 92,584
Brazil 4,674 68,188
Uchina 4,637 83,938
Netherlands 4,566 38,421
Uturuki 2,992 114,653
Canada 2,851 49,751
Sweden 2,355 19,621
Uswizi 1,699 29,264
Mexico 1,434 15,529
Ireland 1,102 19,648
Ureno 948 24,322
India 939 29,451
Urusi 867 93,558
Peru 782 28,699
Indonesia 773 9,511
Ecuador 663 23,240
Romania 663 11,616
Poland 596 12,218
Austria 569 15,357
Ufilipino 530 7,958
Algeria 437 3,649
Denmark 434 8,851
Japan 385 13,614
Misri 359 5,042
Kashmir inayotawaliwa na Pakistan 312 14,514
Hungary 291 2,649
Jamuhuri ya Dominica 286 6,416
Colombia 253 5,597
Korea Kusini 244 10,752
Ukrain 239 9,410
Jamuhuri ya Czech 225 7,486
Israel 208 15,589
Chile 207 14,365
Norway 206 7,619
Finland 199 4,740
Argentina 197 4,003
Panama 167 6,021
Morocco 165 4,252
Bangaldesha 155 6,462
Saudi Arabia 152 20,077
Ugiriki 138 2,566
Serbia 125 6,630
Moldova 103 3,638
Malaysia 100 5,851
Afrika Kusini 90 4,793
Iraq 90 1,928
Milki za Kiarabu 89 11,380
Luxembourg 89 3,741
Slovenia 86 1,408
Australia 83 6,721
Belarus 79 12,208
Macedonia Kaskazini 71 1,421
Honduras 64 702
Croatia 63 2,047
Bosnia na Herzegovina 63 1,585
Afghanistan 58 1,828
Cameroon 58 1,705
Cuba 58 1,437
Bulgeria 58 1,399
Thailand 54 2,938
Bolivia 53 1,014
Estonia 50 1,660
Lithuania 44 1,344
Burkina Faso 42 635
San Marino 41 538
Nigeria 40 1,337
Andorra 40 743
Tunisia 39 967
Visiwa vya Channel 36 530
Armenia 30 1,867
lbania 30 750
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo 30 471
Niger 29 701
Somalia 28 528
Kazakhstan 25 3,019
Sudan 25 318
Lebanon 24 717
Mali 24 424
Kuwait 23 3,440
Azerbaijan 22 1,717
Isle of Man 21 309
Slovakia 20 1,384
New Zealand 19 1,472
Liberia 16 141
Cyprus 15 837
Uruguay 15 620
Guatemala 15 530
Singapore 14 14,951
Cote d’voire 14 1,164
Kenya 14 374
Martinique 14 175
Latvia 13 836
Meli ya Diamond Princess 13 712
Saint Martin (Eneo la Ufaransa) 13 75
Kosovo 12 510
Guadeloupe 12 149
Ghana 11 1,550
Bahamas 11 80
Qatar 10 11,921
Oman 10 2,131
Iceland 10 1,795
Mauritius 10 334
Venezuela 10 329
Tanzania 10 299
Senegal 9 823
Paraguay 9 230
Bahrain 8 2,810
Uzbekistan 8 1,939
Kyrgystan 8 708
Jordan 8 449
El Salvador 8 345
Congo 8 207
Trinidad and Tobago 8 116
Guyana 8 74
Guinea 7 1,163
Sri Lanka 7 619
Jamaica 7 364
Montenegro 7 321
Costa Rica 6 697
Georgia 6 511
Taipei ya China 6 429
Bermuda 6 110
Togo 6 99
Barbados 6 80
Haiti 6 76
Myanmar 5 149
Mayotte 4 460
Malta 4 458
Sierra Leone 4 104
Monaco 4 95
Zimbabwe 4 32
Gabon 3 211
Ethiopia 3 126
Zambia 3 95
Syria 3 43
Malawi 3 36
Antigua na Barbuda 3 24
Nicaragua 3 13
Djibouti 2 1,035
Maeneo ya Wapalestina 2 342
Aruba 2 100
Libya 2 61
Angola 2 27
Belize 2 18
Meli ya Zaandam 2 9
Equitorial Guinea 1 258
Brunei Darussalam 1 138
Guiana ya Ufaransa 1 124
Cape Verde 1 114
Liechtenstein 1 82
Guinea_Bissau 1 73
Eswatini 1 71
Visiwa vya Cayman 1 70
Benin 1 64
Botswana 1 22
Curacao 1 16
Turks nad Visiwa vya Caicos 1 12
Burundi 1 11
Montserrat 1 11
Gambia 1 10
Suriname 1 10
Mauritania 1 7
Visiwa vya Virgin vya Uingereza 1 6
Kisiwa cha Reunion 0 418
Vietnam 0 270
Maldivers 0 245
Rwanda 0 207
Visiwa vya Faroe 0 187
Gibraltar 0 141
Madagascar 0 128
Cambodia 0 122
Uganda 0 79
Mozambique 0 76
Polynesia ya Ufaransa 0 58
Nepal 0 54
Jamuhuri ya Afrika ya Kati 0 50
Chad 0 46
Eritrea 0 39
Mongolia 0 38
Timor_Leste 0 24
Jamuhuri ya kidemokraia ya watu wa Lao 0 19
Grenada 0 18
New Caledonia 0 18
Fiji 0 18
Dominica 0 16
Namibia 0 16
St St Vincent na Gradines 0 15
Saint Lucia 0 15
Saint Kitts na Vevis 0 15
Visiwa vya Falkland 0 13
Ushelisheli 0 11
Greenland 0 11
Vatican 0 10
Sao Tome and Principe 0 8
Papua News Guinea 0 8
Bhutan 0 7
Sudan Kusini 0 6
Saint Barthélemy 0 6
Milki ya Magharibi mwa Sahara 0 6
Anguilla 0 3
Yemen 0 1

Maelezo haya yanatokana na data za mara kwa mara kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins na huenda yasiangazie hali halisi ya mambo yalivyo katika kila nchi.

Chanzo: Chuo kikuu cha Johns Hopkins (Baltimore, Marekani), maafisa wa eneo

Takwimu zilizowekwa mara ya mwisho 28 Aprili 2020, 19:07 GMT +1

Shirika hilo lenye makao yake Marekani ambalo hutoa msaada wa kibinadamu kote duniani, limesema kwamba mambo mengine kama ukubwa wa nyumba, idadi ya watu, kiwango cha huduma za afya na migogoro ya awali huenda vikaongeza hatari ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona kwa nchi zinazoendelea.

Idadi rasmi ya walioambukizwa ama kufa kwa virusi vya corona katika nchi zinazoendelea ni ya chini lakini kuna uwezekano mkubwa idadi hiyo kiuhalisia ikawa ni ya juu.

Caroline Seguin, anayesimamia miradi ya kimatibabu nchini Yemen kupitia shirika la kimatababu lisilokuwa na mipaka, anasema shirika hilo linaamini kwamba tayari raia wamekufa kwa ugonjwa wa Covid-19 ingawa sio hospitalini.

“Tunaamini kwamba maambukizi ya ndani kwa ndani yanaendelea lakini kiwango cha wanao pimbwa kiko chini sana,” ameiambia BBC.

Virusi vya corona: Kuna hofu ya virusi katika kambi ya wakimbizi ya Idlib
Image captionVirusi vya corona: Kuna hofu ya virusi katika kambi ya wakimbizi ya Idlib

Bi Seguin amesema Yemen, ambayo iliangaziwa katika ripoti iliyotolewa na shirika la IRC, imeonyeshwa kama nchi iliyo katika hatari zaidi ya kuathirika vibaya na virusi vya corona na kuongeza kwamba tayari nchi hiyo imeathirika vibaya na milipuko mingine ya hivi karibuni kama kuhara na ukambi/surua.

“Mfumo wa afya umeshindwa kabisa kufanyakazi… na bila shaka wizara ya afya haiwezi kukabiliana na virusi vya corona,” amesema.

The post Watu bilioni moja huenda wakaambukizwa Corona duniani kote, Fahamu zaidi appeared first on Bongo5.com.