Watu 16 akiwemo Ofisa wa polisi mwanamke wameuawa katika shambulio la risasi lililoendeshwa na mtu mwenye silaha katika kijiji kidogo cha Nouvelle-Écosse, Mashariki mwa Canada, kabla ya kudhibitiwa na polisi.

Haya ni mauaji mabaya kuwahi kutoka nchini Canada tangu miaka thelathini iliyopita.

Kwa muda wa saa 12 za makabiliano, polisi  ilizingira kituo cha mafuta, na mshambuliaji anadaiwa kuwa ameuawa, huku shambulio la muuaji huyo likigharimu maisha ya watu 16.


Ofisa wa polisi mwanamke mwenye miaka 23 ya uzoefu ni miongoni mwa watu waliouawa.
 

Sababu za mshambuliaji Gabriel Wortman, 51, kutekeleza shambulio hilo hazijajulikana bado.Mshambuliaji alitumia gari linalofanana na magari ya polisi