Janga la corona linampa kila mmoja tajriba yake. Wengine wanajitenga juani, wengine wanachungulia kutoka madirishani.

Watafiti wanasema kwamba wale wanaopoteza kazi zao mara nyingi ni vijana wadogo na wanawake ambao tayari walikuwa na kipato cha chini.

Kwa wafanyakazi wanaoishi kwa kutegemea mapato ya kila siku, kufungiwa kutotoka nje kuna maanisha kwamba itakuwa changamoto kwao kupata mkate wa kila siku.

Ni jambo linalokatisha tamaa lakini sio kitu cha kushangaza kwamba janga hili, kuna uwezekano mkubwa ukafanya watu maskini wakaendelea kuwa maskini zaidi.

Lakini pia nyakati kama hizi zinaweza kuwa nzuri kwa mabadiliko.

Hio haitakuwa mara ya kwanza.

Katika mgogoro wa kiuchumi 2008 usalama wa jamii ndilo suala lililopewa kipaumbele nchini Brazil. Miaka ya 90, barani Asia kulikuwa na mporomoko mkubwa wa kiuchumi uliosababisha kuanzishwa kwa huduma za afya kwa wote nchini Thailand.

Turejelele suala la kuporomoka kwa uchumi Marekani ndo kulikuwa chanzo cha mfuko wa ustawi wa jamii. Vita ya pili ya dunia ilikuwa kichocheo cha mfumo wa Afya wa Taifa nchini Uingereza.

Majanga kama hayo yanaweza kusababisha jamii kufanya maamuzi ambayo awali yalionekana kama jambo lisilowezekana.

Je janga hili la corona linaweza kuwa chanzo cha dunia kuwa sawa kwa kila mmoja?

Kupoteza mamilioni

Hilo ni jambo lililotokea katika kampuni moja ndogo mjini Seattle wiki chache zilizopita.

Katika kampuni ya Gravity payments mapema mwaka huu, ilikuwa inatimiza maadhimisho ya miaka 5 tangu ilipochukua maamuzi ambayo sio ya kawaida.

Mkurugenzi Dan Price alikubali kupunguziwa mshahara wake kwa dola milioni moja ili aweze kulipa wafanyakazi wake kiwango cha chini cha mshahara cha dola 70,000.

Wafanyakazi walifurahia uamuzi huo lakini muda mfupi baadae, dunia ikakumbwa na janga.

Kupitia njia ya video, wiki jana Bwana Price alionekana kusonga na mawazo. Ulikuwa ni muda wa kupata msongo wa mawazo.

“Sijawahi kuumwa na kichwa kiasi hiki,” anasema. “Nimekuwa nikiumwa na kichwa kwa wiki 5.”

Dan PriceDan Price akitabasamu siku za nyuma ambapo mambo yalikuwa shwari.

Eneo la Gravity lipo Seattle, moja ya maeneo yaliyokubwa na virusi.

Huwa inatengeneza kadi za malipo kwa biashara ndogo ndogo na zile za wastani na kupata asilimia kidogo ya malipo.

Wateja wao wengi ni baa, maduka na migahawa ambazo zimeathirika kwa kiasi kikubwa na amri ya kutotoka nje na kulazimika kufunga biashara.

Bwana Price anasema kampuni hiyo ilikuwa ikipata dola bilioni 4 lakini kwasasa inapata bilioni 2 kwa mwezi.

Bwana Price anasema kwamba hakutaka mfanyakazi yoyote kufutwa kazi hasa wakati ambapo wanahitaji mafao ya msingi kama vile kupata huduma bora ya afya.

Lakini pia hakuweza kuongeza kodi kwa wateja wake ambao pia wanapitia wakati mgumu kukabiliana na janga hili. Hakujua tena cha kufanya.

Children holding hands in Brazil

Kuna mafao yanayoweza kupatikana kipindi hiki?

Tunaishi katika kipindi ambacho ni kigumu mno. Wakati ambapo virusi vya corona vimeenea kote duniani na nchi nyingi zimetoa agizo la kusalia ndani.

Ni matumaini yetu kwamba hatua kama hizo zitakuwa za muda mfupi.

Hatahivyo bwana Price anaamini kwamba hatimae kutakuwa na mafanikio.

Kila siku kuna miradi inayoanzishwa kusaidia watu maskini walioathirika na janga la corona.

Utafiti wake unaonesha kuwa kupitia miradi inayohusisha pesa, watu milioni 622 wanastahili kupata usaidizi ili kupunguza athari za corona.

Anasema kuwa baadhi ya serikali zinajitahidi kuhakikisha zinafikia watu maskini.

Morocco na Colombia wanatengeneza video za Youtube kusaidi watu kutuma maombi ya miradi mingie maalum.

Nchini Uganda, baadhi ya wasichana waliovunja ungo walipata mafunzo fulani ili waweze kupata pesa kidogo zilizokuwa zinatolewa.

India imesema kwamba italipa watu milioni 27.5 pesa taslimu ambao wamendikishwa katika mfumo rasmi wa wafanyakazi wa umma.

Aidha, miradi ya serikali ya taifa katika mji mkuu wa Colombia, Bogota inatoa pesa kwa watu nusu milioni iwapo watakubali kusalia majumbani, kutokaribiana, na kutoshiriki kwenye dhulma za kinyumbani.

Hio ni baadhi tu ya miradi inayoendelea katika maeneo mbalimbali ambayo iliyoanzishwa wiki chache zilizopita.

Hata Papa katika hotuba yake aliotoa sikukuu ya Pasaka iliangazia namna ya kukabiliana na janga la corona

Pope Francis at his weekly audience

“Hiki kinaweza kuwa kipindi cha kufikiria kiwango cha mapato ya msingi kwa wote,” alisema,

Matumaini makubwa ni kwamba pindi miradi hiyo ikishaanza kutekelezwa kuna ile itakayosalia milele.

Mbinu zinazotumika kukabiliana na athari za corona ni zipi?

Wakati Dan Price anazungumza na wafanyakazi wenzake kwa njia ya video mwishoni mwa Machi, aliwaelezea kwamba hali sio nzuri.

Bwana Price alizungumzia tatizo la upungufu wa milioni 1.5 katika mapato ya kampuni na kuuliza wafanyakazi mawazo na hatua zinazoweza kuchukuliwa wakati wa kukabiliana na janga kwasababu kampuni inaelekea kudidimia.

Baadhi walisema kwamba wapunguziwe mshahara wengine wakijibu kuwa hatua hiyo haitakuwa sahihi.

Baadhi ya wafanyakazi walikuwa wenzi wao ama mke au mume ndani ya nyumba anayefanyakazi kwingine na tayari alikuwa ameshasimamishwa, wengine ni wazazi wanaolea watoto wao peke yao.

Hatimae, wote walikubali kupunguziwa mshahara.

Jared Spears ambaye alikuwa kwenye timu ya mauzo ni miongoni mwa wafanyakazi 200 walioshiriki kwenye mkutano, alisema hali ilikuwa imefika mwisho.

A group of people depart from a church where food and essential supplies are distributedMarekani, familia zinazohitaji msaada wa chakula zinazidi kuongezeka

Katika kipindi kama hiki, wakurugenzi wengi hukimbilia wafanyakazi lakini wanapothaminiwa haohao ndo wanaoweza kukunusuru, Bwana Spears amesema.

Kwa wanaharakati wanaopinga ukosefu wa usawa, kile ambacho serikali itafanya miezi michache ijayo. Watafanya maamuzi ya ikiwa matajiri, maskini au wale wa daraja la wastani ndo watakaochukua mzigo wa kudodora kwa uchumi.

Na pia inategemea vile janga la corona litakapodhibititwa hasa kwa misingi ya kisiasa,” anasema mwanauchumi Jason Hickel.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

The post Watafiti wadai kuwa majanga makubwa husaidia kuleta usawa kwa watu wote, Watolea mfano Corona na majanga haya appeared first on Bongo5.com.