Watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona wanatibiwa hospitalini – lakini je ni tiba gani wanayopata na imefanikiwa kwa kiwango gani?

Je ni virusi gani hivi?

Virusi hivyo kwa jina Covid-19 vimeripotiwa kuwauawa watu 53,160 kote duniani huku wengine 1.016,401 wakiambukizwa.

Virusi hivi ni vinatoka katika familia ya coronavirus – maambukizi ya kawaida yanayosababisha Flu na dalili za homa ya kawaida , joto mwilini, kikohozi na matatizo ya kupumua.

Watu wengi wanaoambukizwa virusi hivi hupata dalili hafifu na wengi wanatarajiwa kupona kabisa.

Lakini kama Sars na Influenza , virusi hivi vipya vinaonekana kuwa hatari zaidi miongoni mwa watu wazee na wale wanaougua magonjwa mengine.

Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Hakuna tiba, sawa na jinsi hakuna tiba ya homa ya kawaida.

Ni nini kinachotokea hospitalini?

Wale wanaopelekwa hospitalini hupatiwa tiba kwa kukabiliana na dalili walizonazo huku kinga yao ikijaribu kukabiliana na virusi hivyo.

Mgonjwa anapokuwa hospitalini pia ni njia muhimu ya kuzuia virusi hivyo kusambaa, kulingana na Jonathan Ball mtaalam wa virusi katika chuo kikuu cha Nottingham.

Anapokuwa katika hali mbaya, virusi hivyo vinaweza kusababisha homa ya mapafu au uvimbe katika mapafu. Katika hali hiyo mgonjwa hulazimika kupata usaidizi ili kupumua, amesema profesa Ball.

Wagonjwa hupatiwa Oxygen na katika hali mbaya kabisa huwekwa katika vifaa vya kuwasaidia kupumua. Kisa kimoja kati ya visa vinne duniani hudaiwa kuwa kibaya zaidi.

Mgonjwa aliyeanza matatizo ya kupumua kama huyu anahitaji kuwekewa mashine ya kumsaidia kufanya hivyoMgonjwa aliyeanza matatizo ya kupumua kama huyu anahitaji kuwekewa mashine ya kumsaidia kufanya hivyo

“Iwapo mgonjwa anaonesha dalili za kushindwa kupumua wanamsaidia kupumua .Iwapo kuna shinikizo katika baadhi ya viungo vya mwili watausaidia mwili wake kukabiliana na shinikizo hiyo,” kulingana na Profesa Ball.

Wakati mgonjwa anakabiliwa na dalili hafifu, wagonjwa hupata shida kudumisha shinikizo la damu na hivyobasi hupatiwa dawa kudhibiti tatizo hilo.

Mgonjwa pia hutiwa maji mwilini iwapo anaharisha na dawa aina ya ibuprofen hutolewa kumaliza maumivu.

Zhang Dingyu, mkuu wa hospitali ya Jinyintan mjini Wuhan , aliambia chombo cha habari cha China CCTV kwamba wagonjwa waliopona katika eneo hilo walikuwa ‘katika hali nzuri’.

”Wengine huwa na matatizo ya mapafu” , alisema , lakini nina matumaini kwamba watapona .

Je dawa za HIV zinasaidia?

Ijapokuwa hakuna chanjo dhidi ya virusi vya corona , vipimo vinaendelea China kuona iwapo dawa mbili za kukabiliana na virusi zinazotumiwa kutibu HIV -lopinavir na ritonavir – zinaweza kuwa tiba nzuri.

Dawa hizi zimeonekana kusaidia kukabiliana na virusi vya Sars mwaka 2003, baada ya ushahidi kuonesha kwamba wagonjwa wa HIV ambao walikuwa wakitumia dawa na ambao pia wana virusi vya Sars walikuwa na matokeo mazuri.

”Matumaini ni kwamba virusi vya Sars na vile vya corona vinafanana kwa dawa hiyo kuweza kuwa na mafanikio ya kutosha”, profesa Ball alisema.

Iwapo kuna dalili za mapema inaweza kufanya kazi, kwa kuwa dawa hiyo imethibitishwa kukabiliana na dalili kama hizo.

Matumizi ya huruma ni iwapo dawa ambazo hazijaidhinishwa kutibu ugonjwa fulani zinatumika chini ya masharti makali kwa wagonjwa walio katika hali mbaya ama walio katika hali hatari.

 

Chanzo BBC.

The post Wataalamu waeleza jinsi wanavyowatibu wagonjwa wa Corona na kupona licha ya kutokuwa na dawa inayotibu appeared first on Bongo5.com.