Baraza la Wasomi Wakuu la Saudi Arabia ambalo ndilo shirika la ngazi ya juu kabisa la kidini nchini humo, limewahimiza Waislamu kote duniani kufanya maombi yao nyumbani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, kama nchi zao zitahitaji watu kutokaribiana ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Saudı Arabıa | Coronavirus: Saudi grand mufti says Ramadan night ...

Mwezi wa mfungo wa Ramadhan unaanza baadaye wiki hii. Wakati wa mwezi huu, waumini kawaida hujumuika na familia na marafiki na kufanya sala ya jioni katika mikusanyiko mikubwa misikitini.

Taarifa ya Baraza hilo la Wasomi imesema Waislamu wataepuka mikusanyiko, kwa sababu ndiyo chanzo kikubwa cha kusambaa kwa maambukizi na wakumbuke kuwa kuyatunza maisha ya watu ni kitendo kikubwa kinachowasogeza karibu na Mungu.

Mufti Mkuu wa taifa hilo la Kifalme Sheikh Abdulaziz Al al-Sheikh pia anaunga mkono ushauri huo akisema maombi ya Waislamu wakati wa Ramadhan na pia katika sherehe ya Eid al-Fitr vinapaswa kufanywa majumbani kama mlipuko wa virusi vya corona utaendelea.

The post Wasomi wa Dini, Saudi Arabia wahimiza Waislamu kufanya maombi nyumbani wakati wa Ramadhani appeared first on Bongo5.com.