Real Madrid wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund mwaka huu na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutoka Paris St-Germain 2021. (Marca)
Real Madrid pia inakabiliana na Manchester United katika kinyang’anyiro cha kumsajili winga wa England wa miaka 20 Jadon Sancho, ambaye anachezea klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund. (Daily Star)
Borussia Dortmund imetoa dau la Euro milioni 40 sawa na (£34.9m) kumnunua winga wa miaka 20 wa Uhispania na Valencia Ferran Torres, ambaye mkataba wake unamalizika 2021. (Bild, via Sport)
Mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30, atalazimika kupokea paundi £200,000-kwa wiki ikiwa anataka kubadilisha-uhamisho wake wa mkopo Manchester United kutoka klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki Super League ya China, ambako alikuwa nalipwa where he was on £300,000- kwa wiki. (Daily Star)
Chelsea italazimika kulipa £5m ikiwa inataka kumsajili kiungo wa kati wa Derby County wa miaka 19- Muingereza Max Bird, ambaye mchezo wake umemvutia mkufunzi Blues Frank Lampard alipokuwa meneja wa klabu hiyo. (Football Insider)
Paris St-Germain imeungana na Barcelona katika kinyang’anyiro cha kumsaka kipa wa Cameroon na Ajax Andre Onana, 24. (L’Equipe, in French, subscription required)
Kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 32, amekosoa jinsi Barcelona ilivyomfanyia aliposema kuwa alikataa Paris St-Germain mwaka jana kama sehemu ya mkataba ambao ungelimrudisha mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, Nou Camp. (Mundo Deportivo, in Spanish)
Real Madrid ina mpango wa kusalia na mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 22, ambaye ananyatiwa na Arsenal. (AS, in Spanish)
Mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kusalia Barcelona kwasababu hakuna klabu iko tayari kumlipa euro milioni 60 sawa na(£52.3m). (Marca)
Tottenham wanpania kumsajili kiungo wa kati wa wa Uholanzi Lamare Bogarde, 16, kutoka Feyenoord. (Football Insider)
The post Wanaosakwa sokoni na klabu kubwa barani Ulaya hawa hapa appeared first on Bongo5.com.