Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake ya kijamii ya Twitter amesema kuwa Mgonjwa wa Kagera (Ngara) amepona. Hivyo sasa jumla ya waliopona kufikia watatu (3).

”Mungu ni mwema. Na leo pia hatuna case mpya za COVID19. Mgonjwa wa Kagera (Ngara) amepona. Sasa jumla ya waliopona ni 3. Mgonjwa aliebaki wa Arusha vipimo vyake siku ya 9 leo ni Negative. Tutampima siku ya 14 ili kujiridhisha kama amepona. Wengine 15 waliobaki wanaendelea vizuri,” ameandika Waziri Ummy kupitia Twitter.

Image

The post Waliopona Virusi vya Corona Tanzania wafikia Watatu appeared first on Bongo5.com.