Ripoti ya kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins imesema kuwa takriban kesi za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Marekani imefikia 764,265  huku idadi ya vifo ikiwa ni zaidi ya 40,565. 

Barani Afrika, kesi za maambukizi zimefika 21,317 pamoja na idadi ya vifo 1,080 mpaka kufikia leo Aprili 20.

Mbali na hizo takwimu duniani kote inakdiriwa kuwa na kesi 2,408,304  zilizothibitishwa huku waliopona wakikadiriwa kufikia 629,066 na vifo vikikadiriwa kufikia 165,105