Wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28, amewasiliana na Manchester United kuhusu uwezekano wa uhamisho wa nyota huyo msimu huu. (Sport via Metro)

James Rodriguez

Manchester United wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsaka beki wa Birmingham wa miaka 16-Muingereza Jude Bellingham katika mkataba wa awali wa thamani ya £35m. Chelsea na Borussia Dortmund pia wanamng’ang’ania Bellingham. (Sun)

Everton huenda wakamsajili kiungo wa kati wa Aston Villa Muingereza Jack Grealish, 24, wakipata nafasi. Blues kwa sasa wanamtaka mshambuliaji wa Gremio na Brazil, Everton Soares, 24. (Sky Sports)Jack GrealishEverton huenda wakamsajili kiungo wa kati wa Aston Villa Muingereza Jack Grealish

Everton pia wamepiga hatua katika juhudi ya kumsaka beki wa Lille na Brazil Gabriel Magalhaes. Chelsea na Arsenal pia wanamnyatia kiungo huyo wa miaka 22. (Guardian)

Liverpool wanafanya mazungumzo na ya kumsajili kiungo wa kati wa Milan na Croatia Marcelo Brozovic,27. (Libero via Express)

Real Madrid wanampango wa kusalia na Luka Jovic ambaye pia analengwa na Arsenal. Mshambuliaji huyo wa Serbia wa miaka 22, amechezea Real mechi moja pekee msimu huu. (Sport via Sun)Marcelo BrozovicLiverpool wanafanya mazungumzo na ya kumsajili kiungo wa kati wa Milan na Croatia Marcelo Brozovic

Celtic wamewasiliana na Manchester City kuhusu uwezekano wa kumsajili tena winga wa Patrick Roberts kwa £3m. Mchezaji huyo wa miaka 23-ambaye yuko Middlesbrough kwa mkopo pia aliwahi kuichezea Celtic kwa misimu miwili. (Teamtalk)

Barcelona inamtegemea Philippe Coutinho,27, msimu ujao, amesema mkufunzi Quique Setien. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye yuko Bayern Munich kwa mkopo, amehusishwa na tetesi za uhamisho kuenda Chelsea ama Tottenham. (Evening Standard)

Phillipe Coutinho
Mshambuliaji wa Brazil Phillipe Coutinho

Klabu za Ligi ya Premia zitakutana Ijumaa kujadili uwezekano wa msimu huu kumalizika Juni 30. Ikiwa uamuzi huo utaamuliwa kwa kura, basi klabu 14 kati 20 zitahitajika kukubaliana. (Guardian)

Tetesi za soka Alhamisi

Winga wa kimataifa wa Ujerumani na Manchester City Leroy Sane, 24, anakaribia kuhamia Bayern Munich kwa kiasi cha £70m.(Mirror)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili apate fursa ya kuhamia Inter Milan msimu huu. (Gazzetta dello Sport – in Italian)Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier GiroudMshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud

Arsenal inatarajiwa kamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette mwisho wa msimu, huku Atletico Madrid wakipigiwa upato kumnunua kiungo huyo wa miaka 28. (AS – in Spanish)

The post Wakala wa Rodriguez awasiliana na Man United, Everton yajaribu kumng’oa mchezaji huyu hatari pale Aston Villa appeared first on Bongo5.com.