Klabu za ligi ya Premia zimesema kuwa zitaendelea na ligi hiyo ili kukamilisha mechi 92 zilizosalia msimu huu , lakini hazikusema tarehe rasmi ya kurudi uwanjani katika mkutano siku ya Ijumaa.

Klabu hizo zilitarajiwa kujadiliana kuhusu kurudi uwanjani ifikiapo tarehe 30 mwezi Juni lakini badala yake zikazungumzia kuhusu uwezekano wa kuahirisha mechi hizo.

Ligi hiyo imesema kwamba iko tayari kukamilisha mechi zilizosalia lakini kwa sasa tarehe zote hazijathibitishwa.

Ligi hiyo iliahirishwa tangu Machi 13 kutokana na mlipuko wa virusi hivyo.

Inaeleweka kwamba baadhi ya klabu zilitarajiwa kuzungumzia kuhusu tarehe ya Juni 30 siku ya Ijumaa lakini ikaamuliwa kwamba huu sio wakati wa kufanya hivyo.

”Pamoja na biashara nyengine na viwanda , ligi ya Premia na klabu zetu tunapanga mipango migumu inayoweza kutokea”, ilisema ligi hiyo.

Mkutano wa leo wa wanahisa ulitoa fursa kuzungumzia njia nyingine za kuahirisha mechi hizo, linasalia lengo letu kukamilisha msimu wa 2019-2020, lakini kufikia sasa tarehe zote hazijaamuliwa huku janga la corona likiendelea kuathiri.

Short presentational grey line

Je ligi za Ulaya?

Kufikia sasa hivi ndivyo hali ilivyo:

Ligi ya Ujerumani ya Bundesliga: Klabu zimerudi katika mazoezi lakini msimu ukaahirishwa hadi Aprili

La Liga ya Uhispania: Hakutakuwa na mazoezi hadi harakati za dharura zilizowekwa kuondolewa na rais wa ligi hiyo Javier Tebas amesema ligi hiyo inaweza kurudi uwanjani tarehe 28 mwezi

Ligi 1 ya Ufaransa: Mamlaka ya soka nchini Ufaransa inafikiria kuanzisha ligi hiyo kuanzia tarehe 3 au 17 mwezi June.

Seria A ya Itali: Shirikisho la soka Itali (IFF) linatumai kuanza kuwapima wachezaji mwanzo wa Mwezi Mei ili kujiandaa kuendelea kwa msimu huu.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

The post Vilabu vya Uingereza vyakubaliana ligi kuendelea na sio kufutwa appeared first on Bongo5.com.