Msanii wa Muziki kutoka Marekani Armando Christian Perez maarufu kama Pitbull.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MSANII wa Muziki kutoka Marekani Armando Christian Perez maarufu kama Pitbull  ametoa wimbo unaokwenda kwa jina la " I Believe That We Will Win" kwa maana ya 'Ninaamini Kwamba Tutashinda" ambao ni mahususi kwa ulimwengu mzima ambao kwa Sasa umekumbwa na janga la virusi vya Corona (Covid-19.)

Katika wimbo huo Pittbull ameeleza namna dunia itakavyoshinda dhidi ya virusi vya Corona  ambavyo vimeleta shida ya afya duniani kote.

Aidha katika mashairi ya wimbo huo Pittbull ameeleza kuwa inapokuja hofu unaweza kusahau kila kitu na kukimbia au kukabiliana na kila kitu na kuinuka huku akiwahimiza watu kumtegemea Mungu ambaye ndiye atakayesaidia kuondokana na janga hilo.

Pitbull ameimba; "Sio jinsi unavyoanguka bali ni jinsi unavyoinuka."