Waendesha mashtaka nchini Ujerumani wamesema watu wanne wenye mafungamano na kundi linalojiita dola la Kiislamu IS wamekamatwa kwa kupanga njama za kufanya mashambulizi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Watu hao wanne, ambao ni raia wa Tajikistan pamoja na mwenzao watano ambaye alikamtwa mwaka jana, inaaminika walikuwa wakipanga kufanya mashambulizi dhidi ya kambi za majeshi ya Marekani zilizopo nchini Ujerumani.
Waendesha mashitaka hao wamesema kuwa washukiwa hao pia walikuwa wakiwafuatilia watu wanaoupinga Uislamu kwa lengo la kuwashambulia siku za usoni.
Watu hao walikamatwa hapo jana Jumatano katika miji ya magharibi mwa Ujerumani ya Essen, Neuss, Siegen pamoja na Heinsber.
The post Ujerumani: Wanne wakamatwa kwa kupanga njama za mashambulizi katika kambi za jeshi la Marekani appeared first on Bongo5.com.