Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba China itatumia kila njia ili kumfanya asichaguliwe , akizidisha shutuma zake dhidi ya Bejing wakati ambapo dunia inakabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

Katika mahojiano yaliofanyika katika Ikulu ya Whitehouse na chombo cha habari cha Reuters, amesema kwamba Beijing inakabiliwa na athari chungu nzima kutoka kwa Marekani kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Anasema kwamba China ingeupasha ulimwengu habari za mlipuko wa corona mapema. Bwana Trump yeye mwenyewe amekuwa akikosolewa kwa Jinsi anvyokabiliana na tatizo hilo.

Mlipuko wa virusi vya corona umeharibu uchumi wa Marekani ambao rais Trump alikuwa akitumia kujipigia debe ili kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Bwana Trump ambaye amekuwa akipigana kibiashara na China hakutoa maelezo yoyote ya jinsi atakavyoichukulia hatua kali Beijing.

Aliambia Reuters: Kuna vitu vingi ninaweza kufanya. Tunachunguza kile kilichotokea.

Trump aliongezea: China itafanya kila juhudi za kutaka nipoteze katika uchaguzi ujao. Rais huyo wa chama cha Republican amesema kwamba anaamini kwamba Beijing inataka mpinzani wake mkuu kutoka chama cha Democrat Joe Biden kushinda uchaguzi wa mwezi Novemba.

Bwana Trump pia alikosoa data inayosema kwamba huenda bwana Biden akaibuka mshindi.

“Siamini kura hizo za maoni”, alisema rais huyo. ”Naamini kwamba raia wa taifa hili ni watu werevu. Na sidhani kwamba watamchagua mtu ambaye hawezi kumudu changamoto zao”.

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti mapema kwamba bwana Trump aliwakaripia washauri wake wa kisiasa kuhusu kura ya maoni ilio muonyesha kwamba atapoteza majimbo muhimu.

Rais Xijiping wa China kushoto na Trump kulia

Washauri wake wana wasiwasi kuhisu iwapo Trump ataibuka mshindi katika majimbo muhimu kama vile Florida, Wisconsin na Arizona , huku kundi la kampeni yake likivunja tamaa ya kushinda katika jimbo la Michigan , kulingana chombo cha habari cha AP.

”Siwezi kupoteza kwa Joe Biden, Bwana Trump aliripotiwa akisema wakati alipokuwa akikutana na maafisa wake wa kampeni kupitia mtandao”.

Rais huyo wa Marekani pia aliripotiwa kumkemea meneja wake wa kampeni , Brad Parscale ambaye alikuwa amemtembelea huko Florida.

Alimshutumu bwana Parscale na mare nyengine kusema kwamba atamshtaki , kulingana na chombo cha habari cha CNN na gazeti la Washington Post , ijapokuwa haijulikani iwapo ni kweli atachukua hatua hiyo ya kisheria.

Uchanganuzi

Ukosoaji wa rais Trump dhidi ya China umekuwa ukiendelea na kuongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni.

Alihoji usahihi wa idadi ya vifo nchini humo na hata kusema anaunga mkono maoni kwamba virusi hivyo vilitoka katika maabara mjini Wuhan.

Lakini huo ndio ukosoaji mbaya zaidi kuwahi kutokea kufikia sasa.

Kwa kudai kwamba hatua ya China ya kuchelewa katika kuelezea dunia kuhusu maambukizi ya virusi hivyo kulishinikizwa kisiasa na kulilenga kuimarisha fursa ya mpinzani wake wa kisiasa Joe Biden.

Mapema wiki hii afisa mmoja wa China , Le Yucheng , alihoji jinsi rais anavyolitazama swala lote la mgogoro huu , ambao matokeo yake yataathiri uchumi .

Kwa sasa watu waendelee kutarajia vita vya maneno kati ya mataifa mawili yenye uchumi mkubwa dunaini.

Presentational grey line

Mapema siku ya Jumatano , bwana Trump alisema kwamba hatoongeza masharti ya kutokaribiana katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona yatakapokamilika siku ya Alhamisi.

Masharti hayo ambayo yalitarajiwa kuendelea kwa siku 15 na baadaye kuongezwa tena kwa siku 30 – yaliwasukuma Wamarekani kufanya kazi kutoka nyumbani na kuzuia kujumuika katika mikutano ya watu wengi huku ikiwashauri wale walio na magonjwa mengine kujitenga.

Baada ya takriban mwezi mmoja wa kujitenga ndani ya Ikulu ya Whitehouse, bwana Trump alisema kwamba anapanga kuendelea kusafiri , akianza na ziara ya Arizona wiki ijayo.

Mwanamke akipimwa virusi vya corona

Aliambia wanahabari kwamba anataraji kufanya kampeni kubwa katika kipindi cha miezi ijayo na maelfu ya wafuasi wake.

Marekani kwa sasa ina thuluthi moja ya wagonjwa wote wa virusi vya corona duniani.

Idadi yake ya vifo ni zaidi ya 60,000 – katika kipindi cha wiki sita imepiku idadi ya Wamarekani waliofariki katika vita vya miongo miwili vya Vietnam.

 

Ukosefu wa ajira , ambao wiki chache zilizopita ulikuwa chini sasa umefikia watu milioni 26.

Takwimu mpya zilizotolewa siku ya Jumatano zilionyesha kwamba Uchumi wa Marekani ulishuka kwa asilimia 5 – ikiwa kiwango kibaya zaidi.

The post Trump “China haitaki nichaguliwe Urais awamu ijayo” appeared first on Bongo5.com.