Rais wa Marekani , Donald Trump amesema kuwa uongozi wake utasitisha ufadhili kwa Shirika la afya duniani (WHO).

Amesema WHO imeshindwa kufanya majukumu yake muhimu katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

Ameishutumu Umoja wa mataifa kwa kutoweza kukabiliana na kusambaa kwa janga hili la virusi vya corona ambavyo vilianzia nchini China, na linapaswa kulaumiwa. Bwana Trump awali aliishutumu WHO kwa kuipendelea China.

Aidha rais Trump mwenyewe alikosolewa nchini mwake kwa namna anavyokabiliana na mlipuko huo nchini mwake.

“Ninawapa muongozo utawala wangu kusitisha ufadhili wakati Shirika la afya duniani likiwa linachunguzwa katika majukumu yake yaliyoshindwa kuyatimiza katika kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona ,” Bwana Trump aliwaambia waandishi katika White House.A building of the World Health Organization (WHO) in Geneva, Switzerland, February 6, 2020

Shirika la afya duniani -WHO limeshindwa majukumu yake muhimu na wanapaswa kuwajibishwa, ” aliongeza.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres alisema kuwa wakati huu si wakati wa kukata ufadhili kwa WHO.

Marekani ndio mfadhili mkubwa wa WHO’ anayetoa ufadhili wa kiasi cha dola milioni 400 ambayo ni 15% ya bajeti yake ya mwaka jana.

China ilichangia mwaka 2018-19 karibu dola milioni 76m na yapata dola milioni 10 katika ufadhili, kwa mujibu wa mtandao wa shirika la afya duniani.

Shirika hilo lilitenga kiasi cha dola milioni 675 kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na limeripotiwa kuwa litaongeza fedha hizo hadi karibu dola bilioni moja.

“Mlipuko huu wa ugonjwa wa ovid-19 unatia wasiwasi kama ukarimu wa Marekani umepewa kipaumbele sahihi au la,” rais alisema.

Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona duniani kwa kuwa na wagonjwa 608,377 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo kufikia 25,981.

Rais Trump ameishutumu WHO kwa kushindwa kukabiliana na mlipuko huu ulipoanza kwa mara ya kwanza mjini wa Wuhan.

“Hivi WHO imefanya kazi yake ipasavyo kwa kutumia wataalamu wake wa afya kuchunguza hali ilivyo China na kubaini ukosefu wa uwazi kwa kuwa kuna idadi ndogo ya vifo vilivyotokana na mlipuko huo,” aliwaambia waandishi.

“Tukibaini hayo tutaweza kuokoa maisha ya maelfu ya watu na kuzuia uchumi wa dunia kuanguka. Lakini WHO iko tayari kuiamini China bila kuangalia uhalisia na kutetea hatua zinazochukuliwa na serikai ya China.

Ripota wa White House walinukuu kuwa bwana Trump mwenyewe alisifu itihada za China katika kukabilianna na janga hili na kuhofia hatari ya ugonjwa huo nchini mwake.

Akizungumza akiwa katika busatani ya Rose iliyopo White House, Rais Trump alisema pia mipango ya kuachana na amri hiyo ya kutotoka nje iko ukingonui.

Bwana Trump alisababisha taharuki siku ya Jumatatu kwa kusema kuwa yeye na magavana wa majimbo wana mamlaka ya kuachia watu waendelee na shughuli zao na kurudisha uchumi.

Lakini siku ya Jumanne , alibadilisha muelekeo na kusema kuwa magavana ndio wanawajibika katika hilo.

“Magavana wanapaswa kufanyia kazi suala hilo vizuri sana na kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa weredi , kwa sababu ikitokea ndivyo sivyo watawajibishwa..”

Wataalamu wanakubali kuwa ni magavana ndio wana jukumu la kuweka sheria katika majimbo ya Marekani.

Mapema Jumanne, gavana wa New York Andrew Cuomo alimshutumu rais Trump kwa kuharibu mapambano ya mlipuko huo.

“Hatuna mfalme bali tuna rais,” alisema.

Trump anailenga China

Kwa upande mmoja, hatua zilizochukuliwa dhidi ya virusi vya corona. Utawala uliilaumu haraka shirika la afya duniani kwa kushindwa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo na kudai kuwa ilikuwa inawapendelea China.

Walisema kuwa WHO ilikuwa na utayari mkubwa kuwasaidia China ambayo ilikuwa inawapotosha kwa kuwapa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Na rais Trump alikosolewa na WHO kuhusu maamuzi yake ya kuweka katazo la usafiri dhidi ya China.

Lakini katika hatua nyingine, uamuzi wa kuondoa ufadhili wake kwa WHO ni sehemu ya jitihada za utawala wa Trump kuzuia China kukua kiuchumi.

Mvutano wa viongozi wa China katika mashirika ya kimataifa umedumaza muongozo wa kuwajibika kwa mfumo wa kimataifa katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu wa corona.

Lakini ripoti iliyoandikwa katika jarida la la ‘Wall Street’ imesema kuwa maamuzi hayo yanazua chachu ya mjadala kuendelea kuhusu msaada wa dola za kimarekani unawafikia unawafikia.

Kwa nini shirika la afya duniani linakosolewa?

Si mara ya kwanza kwa jitihada za WHO kukosolewa katika namna wanavyokabiliana na janga hili.

Mwezi February, WHO ilisema kuwa katazo la kuzuia watu kusafiri halihitajiki ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19 -jambo ambalo lilipuuziwa na wengi.

Mwezi Machi, ilishutumiwa kwa kushindwa kufanya majukumu yake baada ya mafiasa wakuu wa China kukataa kwenda Taiwan kujadili namna ya kukabiliana na mlipuko huo

Kwa sasa, wataalam wa afya wanasema kuwa maelekezo ya uvaaji wa barakoa umewachanganya watu na kushindwa kujua kipi ni sahihi kufanya.

Jimbo la New York lina visa 190,000 na zaidi ya vifo 10,000 vilivyotokana na ugonjwa wa corona. Ingawa kunaonekana kuwa na dalili za idadi ya maambukizi kushuka.

The post Trump atangaza kusitisha ufadhili WHO, adai limeshindwa kutimiza majukumu  appeared first on Bongo5.com.