Rais Trump ameitaka Marekani kuanza kutafuta raslimali kwenye mwezi. Rais huyo alisaini amri inayosema Marekani ina haki ya kutafuta na kutumia raslimali katika anga la juu.

Why does President Trump want to mine on the Moon? - BBC News

Amri hiyo pia ilisema kwamba Marekani haichukulii anga la juu kama sehemu ya kawaida yenye raslimali na hivyobasi, haihitaji ruhusa au kufikia makubaliano ya kimataifa ili kuanza shughuli zake.

Kulingana na Sarah Cruddas, kutafuta madini kwenye mwezi kutasaidia wanadamu kusafiri maeneo ya mbali zaidi katika anga la mbali hadi maeneo ya Mars.

Mwanahabari wa masuala ya anga za mbali anasema kwamba kwenye mwezi kunaweza kuwa na kituo cha mafuta kwasababu kuna kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya fyueli ya roketi kama vile hidrojeni na oksijeni.

Kuwa na kituo cha mafuta katika anga ya mbali kuna maanisha kwamba roketi zinaweza kusafiri mbali zaidi katika anga hiyo bila kuwa na wasiwasi ya mafuta yakuisha.

“Ni sawa na kutobeba jiko lako wakati unakwenda likizo. Hatustahili kubeba kila kitu wakati wa safari ya anga za mbali,” Sarah ameiambia Radio 1 Newsbeat.

Kutakata kufahamu kwa undani zaidi ni muhimu kwasababu anga ya mbali kuna raslimali nyingi ambazo zinaweza kutumiwa kwa manufaa ya dunia.Donald TrumpHuu ni uamuzi wa hivi punde uliofanywa na rais – mwaka uliuopita alibuni kikosi cha anga za juu

Profesa Benjamin Sovacool anasema kwamba dunia inaelekea katika kujikita kwenye vyanzo vya nishati mbadala kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa na inahitaji raslimali hizo.

“Kwasasa tunaelekea kumaliza raslimali tulizonazo,” Benjamin amesema.

Benjamin ni Profesa wa masuala ya nishati katika Chuo Kikuu cha Sussex na anasema kwamba kutafuta raslimali zaidi kwenye anga la juu kunaweza kusaidia kutengeneza bidhaa zengine kama magari yanayotumia nishati ya umeme – ambako katika kipindi cha muda mrefu, litakuwa jambo lenye manufaa kwa mazingira.

Mzozo kati ya Marekani na China

“Chuma kama lithuamu na kobalti – vinavyohitajika – vinapatikana tu nchini China, Urusi au Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Na ni nadra sana kupatikana.”

Anasema kwamba inaweza kuwa changamoto kutafuta raslimali kutoka kwa wauzaji mbalimbali kote duniani ambapo kila mmoja anasheria zake.

“Kutafuta raslimali kwenye mwezi, ambapo zinapatikana eneo moja, inaweza kufanya kazi hiyo kuwa rahisi,” ameongeza.

Sarah anasema kutafuta raslimali hizo duniani katika maeneo kama Congo, kunafanyika chini ya mazingira hatari ya kuogofya”.

Lakini Benjamin ameonya kwamba anga la juu sio suluhisho ya muda mfupi kwa changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Moja ya sababu ya uamuzi wa Rais Trump kutafuta madini kwenye mwezi, kunaweza kuwa ukosefu wa nyenzo kwa Marekani ikilinganishwa na mataifa mengine duniani.

“Marekani imepoteza dira – nchi zingine kama vile China na Urusi ziko mbele,” anasema Benjamin.

Nyenzo zinazotengenezwa na China zinapatikana kote duniani.

“Itakuwa jambo la kuvutia kwa watu kama Rais Trump ikiwa utaweza kupata raslimali katika maeneo ambayo haichukui – kama anga la mbali.”

Kumekuwa na wasiwasi kati ya Marekani na China tangu rais Trump kuingia madarakani na Benjamin anasema hii ni fursa kwake kuonesha utawala na uongozi.

Sheria inasemaje?

Amri ya Rais Trump ni wazi kwamba sheria ya kimataifa haitatumika katika juhudi za Marekani kwenye anga la mbali – lakini sheria kuhusu kile mwanadamu anaweza kufanya katika eneo jingine mbali na dunia hazijabainishwa waziwazi.

“Sheria ya anga za mbali inaendelea kupanuka, bila shaka itabadilika kadiri muda unavyokwenda,” Sarah anasema.

Hakuna nchi “inayoweza kusema kwamba inamiliki mwezi”, lakini kwasasa ni kama sharia ya baharini: “Unakapofika huko, ukaona kit una kuchukua – ni chako.”

Benjamin anasema kwamba kutozungumzia anga la mbali ni jambo lisiloepukika kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa kunakoendelea kutokea duniani kwasasa.

“Moja ya hoja za watu ni kwamba anga la mbali ndio eneo pekee la kwenda kwasababu mwisho wa siku mwanadamu ataharibu kabisa dunia,” anasema.

“Mtanzamo uliopo ni kwamba anga la mbali ndio hatma pekee ua mwanadamu iliyosalia.”Satellite ikiwa anga za juuMtambo wa Satellite unaotoa habari kuhusu sayari

Je hilo linawezekana?

Kulingana na Sarah, “teknolojia ipo” na maendeleo yake ni ya haraka mno kwasababu kuna kampuni nyingi za kibinafsi zinazohusika.

“Awali, ilikuwa tu ni serikali ndo yenye kufadhili miradi kama hiyo. Lakini kwasababu ya kampuni mbalimbali na watu binafsi, pesa zinapatikana na pia wanashauku ya matokeo,” ameiambia Newsbeat.

“Tutashuhudia maenndeleo makubwa katika masuala kama utafutaji madini mwenye mwezi, sayari ndogo, baharini, na wanadamu kutembelea Mars. Hivi vyote vinawezekana katika karne hii.”

Lakini Benjamin anasema ni muhimu vilevile kutumia teknolojia ya zilizopo katika mchakato wa uchimbaji madini duniani.Mfumo wa SolarAngani kuna madini katika ambayo inaweza kuimarisha maisha duniani

“Utafutaji madini kwenye mwezi ni kitu ambacho sio rahisi kufikia,” amesema.

“Kwahiyo, kwanza tafuteni madini yanaohitaji kwa haraka kama vile gesi na maji ya kina cha chini kabisa. Baada yah apo munaweza kupanda hadi kiwango kingine.”

Inavyoonekana utafutaji raslimali kwenye mwezi kunaweza kutoka miaka 10 hado 15 ijayo”, n ahata wakati huo hatma yake itategemea vigezo vingine kama vile pesa na raslimali.

Mwisho wa wote, itakuwa ni kupiga hatua nyengine kubwa, amesema Sarah.

“Ukiangalia juu kwenye mwezi, tunatazama nyota. Ni sehemu ya kuendeleza shughuli za mwanadamu zaidi na duniani.”

The post Trump aitaka Marekani kuanza kuchimba madini Mwezini appeared first on Bongo5.com.