Mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Ujerumani Timo Werner ameonekana akijiandaa kwa uhamisho kuelekea ligi kuu ya England kutokana na kuanza masomo ya lugha ya kiingereza, huku Liverpool na Chelsea wakiwa wanamtaka mchezaji huyo, 24. (Mirror)

Liverpool given '65%' chance to sign Timo Werner by BILD

Liverpool imepewa asilimia 65% ya uwezekano wa kumsajili nyota huyo wa RB Leipzig, Timo Werner. Mbali na Liverpool mshambuliaji huyo anahusishwa na Bayern Munich ikiwepewa asilimia 15%  za uwezo wa kunasa saini yake, Real Madrid 10% na Chelsea wakiwa na asilimia 5% za kumnasa.

Real Madrid wanajiandaa kumbakisha Gareth Bale kwenye msimu ujao. Winga wa Wales, anaonakana kuwa na uhakika kuondoka kwenye klabu hiyo kwa sababu ya mahusiano yake yasiyo mazuri na kocha Zinedine Zidane. (Sun)

Chelsea iko mbioni kumsajili kiungo wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye anacheza katika kikosi cha Bayern Munich kwa mkopo. (Sun)

Philippe Coutinho

Tottenham wanakusudia kumsajili beki wa kati Issa Diop, 23 na mshambuliaji wa Wolves na Mexico, Raul Jimenez, 28, katika uhamisho wa gharama ya pauni milioni 96.9. (Football365)

Wakala wa Jorginho anasema kuwa wataingia kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya na Chelsea baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa kiungo huyo, 28 ,atamfuata kocha wa zamani Maurizio Sarri huko Juventus. (Calciomercato – in Italian

)Timo Werner

Timo Werner aanza kujifunza Kingereza

Real wanajiandaa kutoa ofa ya mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 22, kwenda Napoli likiwa ni jaribio la kushusha gharama ya pauni milioni 70 ya mchezaji wa miaka 24 Fabian Ruiz ambaye ananyemelewa na Manchester City.(Mail)SanchoSancho

Winga wa England na klabu ya Dortmund Jadon Sancho, 20, ambaye anahusishwa na taarifa za kuhamia Manchester United ilikuwa ahamie United kutokea Manchester City mwaka 2017. (Mirror)

Mlinda mlango wa lIverpool Loris Karius, 26, anaweza kujiandaa kurejea mapema Anfield akitokea Basiktas ya Uturuki baada ya kulalamiko kwa Fifa kuhusu watu kutolipwa mishahara na timu yake anayoichezea kwa mkopo. (Evening Standard)Cesc Fabregas anapanga kwenda kumalizia mpira Marekani

Cesc Fabregas

Kiungo wa Monaco Cesc Fabregas, 32 , amedokeza mpango wa kuhamia LIgi kuu ya Soka Marekani, akisema yeye ni mpenzi wa ligi hiyo. (Sun)

Mchezaji wa zamani wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Newcastle Warren Barton anafikiri kuwa wamiliki wapya wa klabu hiyo watamfukuza kazi kocha Steve Bruce na Mauricio Pochettino, kocha wa zamani wa Spurs kuchukua nafasi yake.(Express)

The post Timo Werner aingia ‘Tuition’ kujifunza Kiingereza kutua Liverpool ya Jurgen Klopp, wengine sokoni appeared first on Bongo5.com.