Mkuu wa Uhamiaji mkoani Kagera Pendo Butenghe, amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa – Bukoba, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa Azam tv, Akizungumza na mwandishi wetu, Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fush, amesema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kushuka sukari mwilini.

Amesema wanasubiri mwongozo wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na makao makuu ya Uhamiaji kujua taratibu za msiba na maziko.

The post TANZIA: Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kagera afariki dunia, Chanzo chaelezwa appeared first on Bongo5.com.